Moto Hauzimwi

Idadi ya mastaa katika ‘The Blue Mauritius’ yaongezeka

Idadi ya mastaa wakaoonekana katika filamu ya ‘The Blue Mauritius’ imeshafikia 19 huku staa wa filamu maarufu ya ‘Captain America’ Anthony Mackie akipata shavu hilo.

Filamu hiyo inayotarajiwa kuanza kutengenezwa ifikapo mwaka 2018 mwezi March katika  nchi kadhaa ikiwemo Afrika Kusini, Berlin, London, Paris, Acapulco na Mexico . Vile vile filamu hiyo itagharimu kiasi cha dola milioni 20 mpaka sasa katika utengenezaji wake.

Jina la Makie limekuja ikiwa ni wiki kadhaa toka CEO wa D Street Media Group, Dexter Davis kutangaza majina ya washiriki wengine wakiwemo Idriss Sultan na Ernest Napoleon waliowahi kuigiza ya pamoja ‘Kiumeni’.

“Amazing news !!! ???.. Welcome on the team Anthony Mackie, while we’re shooting this movie if you get mugged and the thief runs with only your shoe laces just know it wasn’t me collecting?.. Big big big massive thanks to my executive producer #DexterDavis for giving me the chance to work with these amazingly super great Hollywood stars,” ameandika Idriss kupitia Instagram.

“Finally! Super “A list” actor Antony Mackie known for “Avengers”, “Captain America” and “The Hurt Locker” joins the $20 million Blue Mauritius super cast shooting in Cape Town in March ?????????????????,” ameandika Ernest kupitia Instagram.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW