Aisee DSTV!
SwahiliFix

Idadi ya timu zinazoshiriki Ligi Kuu Soka Tanzania Bara kupunguzwa

Msimu huu 2019/20 utakuwa ndio msimu wa mwisho kwa ligi kuu soka Tanzania Bara kuwa na timu 20 zinazoshiriki.

Hayo yamesemwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura na kudai kuwa mfumo wa Ligi Kuu Soka nchini utabadilika kwa kubakiza timu 16 pekee.

Kwa msimu wa 2020/21 timu zitapungua na kubaki 18, na msimu wa 2021/22 timu zitapungua na kubaki 16 kama ilivyokuwa zamani.
Wambura amesema kwa msimu huo zitashuka timu nne moja kwa moja daraja la kwanza, zitakazo kuwa nafasi ya 17, 18, 19 na 20 huku timu zilizoshika nafasi ya 15 na 16 zikicheza mchujo na mbili za daraja la kwanza.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW