Aisee DSTV!

Idadi ya waliofariki ajali ya moto mkoani Morogoro yaongezeka, Utambuzi wa miili ya marehemu na mazishi kufanyika leo (+video)

Idadi ya watu waliofariki kwenye ajali ya moto mkoani Morogoro imeongezeka kutoka idadi ya watu 68 iliyotangazwa asubuhi na Waziri Muhagama hadi 69, Hii ni baada ya majeruhi mmoja kufariki njiani wakati akisafirishwa kutoka Morogoro kwenda Dar es salaam kwa matibabu zaidi.

Kwa mujibu wa taarifa ya awali iliyotolewa awali na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Uratibu na Bunge Mhe. Jenista Muhagama, amesema baadhi ya mazishi yanatarajiwa kuanza kufanyika leo Jumapili tarehe 11 Agosti, 2019.

Waziri Muhagama amesema maandalizi ya mazishi yameshakamilika ikiwemo uchimbaji wa makaburi na vifaa vyote vya mazishi vimeshanunuliwa na watazikwa katika makaburi ya Kola hill mjini humo.

Kwa upande mwingine, Rais Dkt. Magufuli ametangaza siku 3 za maombolezo ya kitaifa kuanzia  jana Agosti 10, 2019 kufuatia vifo vya watu 69 mpaka sasa vilivyosababishwa na ajali hiyo ya kuungua kwa Lori la mafuta lililopinduka Mjini Morogoro.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW