Habari

Idara ya Habari (MAELEZO) yapokea Kamusi Kuu ya Kiswahili

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Dkt. Hassan Abbasi amekabidhi Kamusi Kuu ya Kiswahili kwa Watumishi wa Idara ya Habari (MAELEZO) katika ofisi za Idara hiyo.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dkt. Hassan Abbasi na Mkurugenzi Sehemu ya Huduma za Habari na Picha, Rodney Thadeus

Dkt. Abbasi amekabidhi Kamusi hiyo leo katika ofisi zake zilizopo Jijini, Dar es Salaam ambapo amesema mojawapo ya jukumu la idara hiyo ni kuhabarisha Umma, hivyo kamusi hiyo itakuwa msaada mkubwa katika uandishi wa habari za kila siku.

“Kamusi hii ina maneno mpaka yaliyoanza kutumika hivi karibuni, kama vile bajaji. Pia ina misamiati mingi ambayo haitumiki, hivyo kwa kuitumia kamusi hii kutaongeza idadi ya misamiati ya Kiswahili kwa watumiaji wa lugha ya Kiswahili,” amesema Dkt. Abbasi.

Aidha Dkt Abbas ameitaka Idara ya Habari kuitumia Kamusi hiyo kama nyenzo muhimu katika kutangaza lugha ya Kiswahili ndani na nje ya nchi pamoja na kutumia misamiati mipya.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents