Burudani ya Michezo Live

Idara za Ujasusi China, Urusi na Korea Kaskazini zapigwa marufuku EU

Umoja wa Ulaya (EU) umeziwekea China, Urusi na Korea Kaskazini vikwazo kwa kuwapiga marufuku maafisa wa idara za ujasusi za nchi hizo kuingia katika nchi za Umoja wa Ulaya.

EU sanctions Russian intelligence, North Korean, Chinese firms ...

Umoja wa Ulaya umechukua hatua hiyo kutokana na idara hizo kutuhumiwa kushiriki katika shughuli za udukuzi wa kimtandao duniani kote.

Idara hizo za ujasusi zinatuhumiwa kujaribu kufanya udukuzi kwenye shirika la kudhibiti silaha za nyuklia. Waliowekewa vikwazo hiyvo ni maafisa sita na taasisi kadhaa za nchi hizo tatu.

Na kwa ajili ya kujihami dhidi ya hujuma za kimtandao Umoja wa Ulaya ulipitisha utaratibu wa kisheria wa kuuwezesha kuweka vikwazo. Vikwazo vya Umoja wa Ulaya pia vitahusu kuzuia mali za watu na hata za taasisi.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW