Habari

Idd Azzan aripoti polisi mchana wa leo, afunguka kuhusu tuhuma zinazomkabili

Aliyekuwa mbunge wa Kinondoni, Idd Azzan ameripoti polisi leo asubuhi baada ya kuambiwa afanye hivyo.

Akiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam, Azzan amesema baada ya kuripoti kama alivyotakiwa ameruhusiwa na kuelezwa kuwa aende katika kituo hicho baadaye.

Azzan amesema tangu watu waanze kumzungumzia kuhusiana na dawa za kulevya ni muda mrefu na hivyo amezungukwa na maadui wengi.

“Mimi tangu nianze kuzungumzwa sijaanza leo, wanasikiliza kwenye mitandao ya kijamii, hawajui mimi nina maadui wangapi ambao wananizunguka. Utakuta mtu tu ananitaja kwa chuki zake,” amesema Azzan.

Amesema polisi walienda nyumbani kwake kupekuwa na hawakupata kitu chochote. “Nasubiri hiyo baadaye wataniambia kitu gani”

Wakati huo huo, Mchungaji Josephat Gwajima aliyedai angekwenda kuwaona wenzake waliosalia polisi, naye pia ameripoti polisi saa 10.46 asubuhi

Msaidizi wa askofu huyo amesema Gwajima ametakiwa kuripoti tena mchana huu.

Source: Mwananchi

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents