Burudani

Idris: Sina dhumuni la kumkashifu yeyote aliyetoa mimba

Mchekeshaji Idis Sultan ameamua kuwatia moyo wanawake wote ambao hawajapata watoto licha ya kuhangaika kwa kipindi kirefu, na kutahadharisha ujumbe wake huo, hauja lenga kumkashifu mtu yeyote au kumbagua.

Idis Sultan

Kupitia mtandao wa instgram, Idris ameandika, “Naomba nianze na kuomba samahani kwa niaba ya wote waliokusahau, tumejisahau sana na tupo chini ya miguu yako. Kuna anayesoma akidhani namuongelea mama yangu mzazi ila sio. Namuongelea mama ya dunia, mama aliyeizalia dunia, mama anayepigana kupata mtoto bila mafanikio, mama aliyepoteza watoto, mama aliyeharibika mimba, mama anayeangalia wenzake wakipata watoto kila kukicha anaalikwa kwenye arobaini za wenzake na anajipa moyo na matumaini ipo siku atawaalika kwenye yake.

“Tumepewa nguvu na uwezo wa kupendana pale tunapoona mapungufu tunapeana moyo. Sina dhumuni la kumkashifu yoyote aliyetoa mimba kwani watoto ni mipango tofauti kwa kila mama. Naomba niweke mwanga kwa yule mama aliyepoteza watoto aliowapangia hadi shule gani watasoma, akanunua hadi kitanda cha mtoto akapamba na chumba kabisa. I need you to know your baby (babies) love you,” ameongeza.

“Mnaweza mkawa hamjapata nafasi ya kuonana ila kwa ule mda mfupi walioishi ndani yako ni the happiest time of their life. Usithubutu hata siku moja kukaa na kufikiria labda ungefanya tofauti isingekua ilivyotokea nooooo you did all you could na Mungu atakupa mengi zaidi. Mama sio lazima uwe na mtoto ila kila unayemfunza kitu, unayemshauri, uliyemsaidia akapata hata chakula wewe ni mama kwake. Jana unaweza ukawa ulilia sana ila leo naomba nikukumbushe kuwa we have your back anytime anyday with un-ending love. Happy mothers day kwako mama,” ameandika Idris.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents