Burudani ya Michezo Live

Idris Sultan amuomba radhi Rais Magufuli ‘Nia yangu ilikuwa ni njema’ (+Video)

Muigizaji na Mchekeshaji maarufu hapa Tanzania, Idris Sultan amemuomba radhi Rais Magufuli kwa kuhariri picha zake, Jambo ambalo limempelekea achukuliwe hatua za kisheria.

Akiongea na waandishi wa habari mapema leo Alhamisi Novemba 14, 2019 asubuhi Jijini Dar Es Salaam, Idris amesema kuwa lengo la yeye kuhariri picha hiyo mtandaoni lilikuwa ni jema na alifanya hivyo kumtakia kheri katika sikukuu yake ya kuzaliwa.

Nia yangu ilikuwa ni nzuri, Lakini katika sanaa kama hii, Nikimkosea mtu yeyote hata kaka yangu hapa, Nikamtakia kheri ya siku yake ya kuzaliwa katika hali ambayo mimi nimehisi ni nzuri. Naye akawa ameiona na akachukizwa na kile nilichokifanya basi sina budi kumuomba radhi. Kwa hiyo kwa post yangu ambayo nimeiweka mtandaoni kama itakuwa imemkera yeye Mhe. Rais mimi naomba nimuombe radhi.“amesema Idris Sultan.

Kwa sasa Idris Sultan anatuhumiwa kwa makosa ya kusambaza habari za uongo chini ya kifungu cha 16 cha sheria ya makosa ya mtandao na kujifanya Rais chini ya kifungu cha 15 cha makosa ya mtandao.

Katika picha hizo alizoziweka mtandaoni, Idris aliweka picha nyingine inayoonyesha sura ya Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Magufuli akiwa amesimama huku amevaa suruali yenye mikanda inayoshikizwa mabegani.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW