Burudani

Idris Sultan atangaza neema kwa Watanzania, aja na mpango wa kuajiri na kulipa mishahara minono

Mchekeshaji maarufu nchini Tanzania, Idris Sultan amefikisha followers milioni 3 kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuahidi nafasi 15 za kazi kama sehemu ya kurudisha kwa jamii.

Idris Sultan

Idris akitoa ahadi hiyo ameandika “nimefikisha 3 million followers instagram na kushukuru jamii kwa hilo nitawapa ajira vijana 15,”.

Kwa upande mwingine, Idris amesema kuwa vijana watano kati ya vijana 15 atawalipa mshahara wa milioni 1 kila mmoja.

Vijana watano kwa kila mmoja milioni. Pata kwa jamii rudisha kwa jamii. We help each other before they help us“ameandika Idris Sultan.

Hata hivyo, Idris Sultan hajaelezawazi kama nafasi hizo za kazi zitapatikana kwa watu wenye sifa gani? na katika kitengo gani?.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents