Kama sio DStv potezea
TECNO Spark 2

Bongo Movie

Idris Sultan na Ernest Napoleon wapata shavu la kuonekana katika filamu ya Hollywood

By  | 

Idris Sultan na muigizaji na mtayarishaji wa filamu za Kiumeni na Going Bongo, Ernest Napoleon wamepata nafasi ya kuigiza katika filamu mpya ya ‘The Blue Mauritius’ ya Marekani.

Filamu hiyo itaanza kutengenezwa mwezi Machi mwakani ambapo kazi hiyo inasimamiwa na kampuni mbili za utengenezaji wa filamu kutoka Marekani ikiwemo D Street Pictures na Benoraya Pictures.

Kwa mujibu wa barua ambayo imetolewa na kampui hizo, imeonyesha kuwa filamu hiyo itatumia kiasi cha dola milioni 17 ambapo ni sawa na shilingi bilioni 38 za kitanzania. Filamu hiyo itafanyika sehemu mbalimbali ikiwemo Cape town, Berlin, London, Paris, Acapulco, Mexico.


Picha za wasanii ambao watashiriki katika filamu ya ‘The Blue Mauritius’

Waigizaji wengine ambao watahusika katika filamu hiyo ni Pearl Thusi (Quantico), Eric Dane (The Last ship/Grey’s anatomy), Gerard Depardieu (Life of pie) John Rhys (Lord of the rings/Indiana Jones) Thomas Kretschmann (Avengers/Kingkong) na Derek de Lint (NCIS/Crossing Lines).

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments

Bongo5

FREE
VIEW