Ifahamu Bima ya Maisha namna ya kufungua na faida zake

CRDB Bima ya maisha inakupa faida ya kuweka akiba kwa malengo ya baadae kama vile elimu kwa uwapendao. Pia, inatoa tulizo la mawazo pale majanga yanapokutokea kwa kukupatia uhakika wa kufanikisha malengo yako uliyoyapanga kwa muda maalum ulioweka.

Faida za Bima ya Maisha

 • Ni lazima uwe na bima ya maisha kabla ya kuanza kuweka akiba
 • Fao la Bima ya maisha litaanza kulipwa kwa wategemezi kuanzia Tsh 3.5m hadi Tsh 50m pale mwenye bima atakapofariki
 • Umri wa kujiunga na bima hii ni kuanzia miaka 18 mpaka 60; na umri wa juu wa bima kuisha ni pale ambapo mwenye bima atafikisha miaka 70.
 • Muda wa kuweka akiba unapaswa kuwa kati ya miaka 7 hadi 18.
 • Kiwango cha chini cha akiba kwa mwezi ni Tsh. 7500 na hakuna kikomo cha kiwango cha juu
 • Malipo yanapaswa kufanywa ndani ya siku 30 baada ya tarehe iliyowekwa lasivyo mkataba huu utasimamishwa
 • Kwa kifo ambacho hakijasababishwa na ajali, malipo yake yatasubiri kwa muda wa miezi sita
 • Wanufaika wa bima watapata faida mara mbili endapo kifo cha mmiliki wa bima kitasababishwa na ajali (Double indemnity)
 • Mnufaika anaweza kuwa mtu yoyote ambaye anaaminika na mmiliki wa bima
 • Endapo mnufaika wa fao la akiba (mtoto) atafariki, nafasi yake inaruhusiwa kuchukuliwa na mtu(mtoto) mwingine
 • Malipo yanaweza kufanywa kwa pesa taslim au kwa malipo yanayojirudia kwa kutumia njia yoyote kupitia akaunti ya Bima

 

Faida za Bima ya Maisha

 

 • Bima ya Maisha – Ikitokea mwenye bima amefariki, fao la maisha litalipwa kwa mkupuo kuanzia Tshs 3,500,000 hadi Tshs 50,000,000. Pia fao la akiba litalipwa lote mara moja kama mwenye bima hajaweka kinga ya kusamehe michango. Endapo mteja ataweka bima ya akiba (WOP), fao lake la akiba litaendelea kulipwa kama mkataba unavyosema.
 • Faida ya kuweka akiba – Ukifika ukomo wa muda uliopanga kuweka akiba, akiba yako yote italipwa pamoja na riba iliyojumuishwa kwa kipindi chote.
 • Kutoa pesa – Unaweza kutoa pesa ndani ya kipindi cha makubaliano lakini hutoruhusiwa kutoa pesa zaidi ya (nusu) 50% ya akiba iliyopo.
 • Kulipa Michango – Ikitokea mwenye bima amefariki au amepata ulemavu wa kudumu kampuni ya bima itaendelea kulipa michango kwa niaba ya mwenye bima kwa kiasi sawa na michango ya akiba ambayo mwenye bima alikuwa akiilipa kabla ya kifo au ulemavu.
 • Ghairisha Mpango wako kwa Muda Uliopanga- Unaruhusiwa kukatiza mpango wako wa bima kabla ya kufika ukomo wa muda uliopanga
 • Uwekezaji zaidi – Unaruhusiwa kuendelea kukuza kiasi cha pesa ambacho tayari kipo kwenye mpango wako wa akiba au bima ya maisha endapo utashindwa kuendelea kuweka akiba au kulipia michango ya fao la maisha.
 • Faida ya kulipwa pesa taslim – Lengo la kulipwa pesa taslim ni kurudisha jumla ya akiba yote uliyoweka ndani ya kipindi cha makubaliano
 • Fao la wajawazito – Lipo fao la likizo la kutokulipa michango hadi mwaka mmoja kwa mwanamke mjamzito
 • Fao la kukosa ajira – Lipo fao la kutokulipa michango hadi mwaka mmoja kwa mwenye bima atakayekosa kazi
 • Jinsi ya kulipa michango – Malipo yanaweza kufanywa kwa utaratibu mmojawapo yaani kila mwezi, kila robo mwaka, kila nusu mwaka au kwa mwaka mara moja

 

Endapo una swali au wahitaji kutuma maombi ya Bima ya Maisha, wasiliana nasi

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW