Fahamu

Ifahamu historia ya aliyekuwa Rais wa pili wa Kenya Daniel arap Moi, Kabla ya kukutwa na Umauti

Ifahamu historia ya aliyekuwa Rais wa pili wa Kenya Daniel arap Moi, Kabla ya kukutwa na Umauti

Kwa zaidi ya robo karne Daniel arap Moi alitawala siasa za Kenya. Yeye alikuwa mwanasiasa aliyetaka kupendwa zaidi na wananchi kuliko alivyokuwa mtangulizi wake, rais wa kwanza wa jamuhuri ya Kenya Mzee Jomo Kenyatta.

Hata hivyo alishindwa kuvunjilia mbali utawala wa kiimla wa Jomo Kenyatta na badala yake yeye mwenyewe akajikuta katika hali ya kuwadhulumu wapinzani wake wa kisiasa.

Alibatizwa jina la “Profesa wa Siasa” kwa vile alivyoweza kukabiliana na wapinzani wake. Hata hivyo utawala wake ulimalizika na sifa mbaya kwa kuwa Serikali yake ilidumaza uchumi na ufisadi ukashamiri.

Moi alizaliwa Septemba 2, mwaka 1924, katika jamii ya wakulima katika kaunti ya Baringo, katikati magharibi mwa Kenya.

Jina lake la kwanza lilikuwa Toroiticha arap (mwana wa) Moi lakini baadaye akabatizwa katika Ukristo na kupewa jina la Daniel. Alipewa jina hilo la Wamishenari Wakristo akiwa mwanafunzi.

Mjumbe

Moi alikuwa mmoja wa mwanasiasa wachache mashuhuri waliofanikiwa, ambaye hakutoka katika mojawapo ya makabila mawili makubwa nchini Kenya – Wajaluo na Wakikuyu. Alitoka jamii ndogo ya Tugen, mojawapo wa makundi yanayounganisha kabila kubwa la Wakalenjin.

Alianza kufanya kazi kama mwalimu mwaka wa 1945 katika shule ya African Government School na mwaka mmoja baadaye akiwa na umri wa miaka 22 akateuliwa kuwa mwalimu mkuu.

Bw Moi alipinga Katiba Mpya wakati wa kura ya maamuzi ya mwaka 2010Bw Moi alipinga Katiba Mpya wakati wa kura ya maamuzi ya mwaka 2010

Baada ya kuhamishwa mara mbili alirudi Kapsabet mwaka 1954 akiendelea kushikilia cheo cha mwalimu mkuu, kazi ambayo aliifanya hadi mwaka 1957.

Hakushiriki kwa vyovyote vile katika harakati za vita vya Mau Mau dhidi ya wakoloni, lakini alipendelea kundi hilo ambapo alitaka sana Kenya kupata uhuru kutoka kwa Uingereza.

Wakati wa mapambano hayo aliwapa makaazi wanachama watano wa Mau Mau kwenye mojawapo wa shamba lake kwa majuma kadhaa.

Machi 1957 Moi alikuwa mmoja wa watu weusi wanane waliochaguliwa kuwa wanachama wa Bunge la Ukoloni kwa Kiingereza Legislative Council ambalo kwa kifupi lilifahamika kama LegCo.

Mapema mwaka 1960 alikuwa mmoja wa wajumbe walioteuliwa kuhudhuria mkutano katika Lancaster House jijini London, ambapo Katiba mpya iliandaliwa na kuwapa Waafrika viti vingi katika Bunge.

Mwaka 1961 aliteuliwa kuwa Waziri wa Elimu, na katika baraza la mawaziri la muungano wa vyama vya kisiasa vilivyoshirikisha Kanu (Kenya African National Union), Kadu (Kenya African Democratic Union – chama cha Moi) baadaye aliteuliwa kuwa Waziri wa Serikali za Mitaa.

Usalama wa taifa

Wakati huo alishiriki katika mikutano mingi iliyokuwa ikiandaa Kenya kwa ajili ya kukabidhiwa uhuru.

Lengo lake kwa wakati huu lilikuwa kuundwa kwa Serikali ya majimbo ambapo serikali hizo ndogo zingelinda maslahi ya makundi ya wachache nchini.

Kenya baadaye ilipata Uhuru mwaka 1963 na Jomo Kenyatta akawa Waziri Mkuu, naye Moi akateuliwa kuwa Waziri kivuli wa kilimo katika muungano wa upinzani. Siasa za Kadu zilidorora kisha chama hicho kikavunjiliwa mbali.

Wengi wa viongozi wengi wa Kadu, Moi akiwemo, walijiunga na chama tawala cha Kanu

Jomo Kenyatta
Moi alikuwa mshirika wa karibu wa mwanzilishi wa taifa la Kenya Jomo Kenyatta

Mwishoni mwa mwaka uliofuata, wakati Jomo Kenyatta alipotawazwa kuwa Rais, Moi aliapishwa kama Waziri wa mambo ya ndani.

Hiki kilikuwa cheo muhimu kwa sababu yeye sasa alisimamia idara ya polisi na pia wajibu wake ulikuwa kudumisha amani na usalama wa kitaifa.

Akiwa bado anashikilia Wizara hiyo mwaka 1967 aliteuliwa kuwa Makamu wa Rais na Naibu mwenyekiti wa chama cha wabunge wa Kanu.

Wakati akishikilia Wizara hiyo mataifa mengi ya kigeni yalikiri kuwa Kenya lilikuwa mojawapo ya mataifa yaliyokuwa na wafungwa wachache sana wa kisiasa.

Ilikubalika pia kuwa hakukuwa na dhuluma na ukandamizaji kisiasa nchini kama ilivyokuwa katika mataifa mengine yaliyokuwa yamepata Uhuru.

Wizara mpya

Wakati Kenyatta alipofariki Agosti mwaka 1978, Moi aliyekuwa makamu wa Rais alichukua wadhifa wa kaimu Rais. Mara tu alipotwaa madaraka hayo alisema kuwa ataendelea na uongozi wa Kenyatta ulioegemea uongozi wa mataifa ya Magharibi, angefuata nyayo.

Mnamo Oktoba alichaguliwa kwa wingi wa kura kuongoza chama cha kisiasa cha pekee nchini Kenya wakati huo ambapo alichaguliwa pia kuwa Rais wa Pili wa Kenya.

Baada ya uchaguzi kufanywa Novemba mwaka uliofuata alifanyia Serikali yake mabadiliko makubwa ambayo yalikuwa hayajashuhudiwa tangu Kenya kujinyakulia Uhuru mwaka 1963.

Alifanya kila juhudi kuimarisha uwezo wa Rais ili anufaike zaidi kwa madaraka.

The Queen & Daniel arap Moi
Akiwa na Malkia Elizabeth kiongozi huyo wa Uingereza alipozuru Kenya mwaka 1983

Wizara mpya kama vile za Mali ya Asili na mazingira zilibuniwa na yingine kama vile za kilimo ziligawanywa.

Agosti 1982 kulitokea jaribio la mapinduzi lakini lilizimwa na wanajeshi waaminifu kwake.

Baadaye mwezi huo Rais alivunjilia mbali kikosi cha jeshi la wanahewa, ambao wengi wao waliongoza jaribio hilo la mapinduzi.

Hali ya wasiwasi

Tukio hilo lilimpa nafasi Rais Moi kuimarisha madaraka yake kwa kuwatimua wote walioshiriki au kushukiwa kushiriki katika jaribio hilo la mapinduzi.

Alihalalisha kuwepo kwa chama kimoja nchini kwa kubadilisha katiba kuweka hilo bayana.

Watu wote waliopinga Kenya kufanywa rasmi kuwa taifa la chama kimoja cha kisiasa walikandamizwa.

Wakati uhasama kati ya mataifa ya Magharibi na Mashariki ulipopungua, umuhimu wa Kenya kuwa muhimu katika juhudi za kupambana na Ukomunisti nchini Ethiopia na Tanzania ulipungua.

Hisia za uthabiti ambao serikali yake ilijivunia zilianza kupungua na wasiwasi ukazuka kutokana na ukatili na ukandamizaji wa wanasiasa wa upinzani.

Idadi ya wafungwa wa kisiasa iliongezeka na Moi alihakikisha vyombo vya habari havitangazi mambo yanayokosoa Serikali yake, huku akiminya uhuru wa kujieleza.

Miaka ya 90 aliwatimua mamia ya maelfu ya watu wengi manyumbani kwao katika Mkoa wa Bonde la Ufa na mamia wakauawa katika mapigano ya kikabila. Wengi wa waliotimuliwa walikuwa wa makabila yaliyoaminika kuwa kwenye upinzani.

Jamii ya kimataifa ilisitisha misaada, iliyokuwa ikitoa kwa Kenya kwa urahisi awali, ili kuhakikisha kunafanyika mageuzi ya kiuchumi, kijamii na kisiasa.

Maneno yake.

Uchunguzi

Miongoni mwa mabadiliko yaliyofanywa nchini wakati huo ni kufanya Kenya kuwa taifa la vyama vingi vya kisiasa. Moi alifaulu kurejesha vyama vingi vya kisiasa lakini akatumia ujanja wa kuyagawa makabila mbalimbali nchini na kushinda uchaguzi miaka ya 1992 na 1997.

Hata hivyo utawala wa Rais Moi ulidumaa kiuchumi na Serikali yake ilikuwa na ufisadi mkubwa hivi kwamba Shirika la Fedha duniani (IMF) na Benki ya dunia (WB) walikataa kutoa mikopo kwa Kenya.

Kashfa kubwa ya rushwa nchini Kenya ilifichuliwa mwaka 1992.

Kashfa hiyo iliyojulikana kama Goldenberg ilihusu kampuni ijulikanayo kama Goldenberg iliyolipwa zaidi ya Pauni za Uingereza milioni 400 kama ruzuku ya kuuza dhahabu na almasi iliyodaiwa kutoka Kenya katika mataifa ya kigeni.

Katika picha hii iliyopigwa Mei 12, 2011, Rais Mstaafu Daniel arap Moi anaonekana akiwa na viongozi wengine akiwemo Rais Mwai Kibaki, Ras wa Zimbabwe wakati huo Robert Mugabe, Jakaya Kikwete wa Tanzania na Yoweri Museveni wa Uganda wakati wa kuapishwa kwa kiongozi huyo wa Uganda.Katika picha hii iliyopigwa Mei 12, 2011, Rais Mstaafu Daniel arap Moi anaonekana akiwa na viongozi wengine akiwemo Rais Mwai Kibaki, Ras wa Zimbabwe wakati huo Robert Mugabe, Jakaya Kikwete wa Tanzania na Yoweri Museveni wa Uganda wakati wa kuapishwa kwa kiongozi huyo wa Uganda.

Ilichukua miaka 14 kabla ya mashtaka kufanywa dhidi ya washukiwa kukiwemo mkurugenzi wa kampuni hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, na Naibu Mkurugenzi mkuu wa zamani wa Benki Kuu ya Kenya.

Uchunguzi rasmi ulionyesha kuwa Rais Moi lazima alifahamu kilichokuwa kinaendelea lakini aliendelea kukanusha kushiriki katika kashfa hiyo muda huo wote na hakushtakiwa kwa lolote.

Katika Uchaguzi wa 2002, ambao Moi alizuiwa kushiriki kikatiba, alidharauliwa sana hivi kwamba gari lake lilitupiwa matope. Chama chake tawala kilitimuliwa madarakani na raia walionyesha Rais Moi madharau ya wazi.

Mwaka 2007 Rais Kibaki alimteua Rais Moi kuwa Balozi Maalumu wa Kenya nchini Sudan Kusini, katika taarifa ambayo Kibaki alisema Rais Moi ana “ujuzi mwingi na ufahamu wa masuala ya Afrika na pia kutokana na sifa zake kama Mzee wa Taifa.”

Bw Moi alipinga Katiba Mpya wakati wa kura ya maamuzi ya mwaka 2010Haki miliki ya pichaAFP/GETTY IMAGES
Image captionBw Moi alipinga Katiba Mpya wakati wa kura ya maamuzi ya mwaka 2010

Moi alitengwa kisiasa na watawala siku zake za mwisho, na aliishi maisha yake bila kuonekana kwenye hafla za umma hadharani.

Mwaka 2010, wakati wa kampeni za kuidhinishwa kwa Katiba Mpya, Bw Moi aliungana na wanasiasa wengine na viongozi wa makanisa kupinga katiba iliyopendekezwa.

Hata hivyo, upande wao ulishindwa kwenye kura ya maamuzi kuhusu katiba hiyo tarehe 4 Agosti.

Wakati wa muhula wa pili wa utawala wa Rais Uhuru Kenyatta, mwanasiasa aliyemwingiza yeye kwenye siasa na kumteua kuwa mgombea wa Kanu alipokuwa anaondoka madarakani, Bw Moi alikuwa mara kwa mara akitembelewa na wanasiasa na maafisa wakuu serikali nyumbani kwake Kabarak.

Chanzo BBC.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents