Afya

Ifahamu Hospitali iliyozalisha watoto zaidi ya 100, Kutoka kwa wanawake wenye Corona

Zaidi ya watoto 100 wenye afya wamezaliwa kutoka kwa wanawake wenye maambukizi ya virusi vya corona katika mji wa magharibi mwa India wa Mumbai.

Watatu kati ya watoto 115 walizaliwa kwa akinamama wenye virusi katika hospitali kuu ya Manispaa ya Lokmanya TilakĀ  – katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita ,awali walipatikana na Covid-19, lakini vipimo vya madaktari vilionyesha kuwa hawakua na virusi, wamesema madaktari.

Wanawake wengine wawili wajawazito walifariki dunia hospitalini, mkiwemo mmoja ambaye alikufa kabla ya mtoto wake kuzaliwa.

Huku ukiwa na watu takriban 24,000 walioripotiwa kuambukizwa corona na zaidi ya vifo 840 hadi sasa, mji mkuu wa biashara na burudani wa Mumbai umekua ni kitovu cha Covid-19.

Zaidi ya nusu ya watoto walizaliwa kwa wanawake walioathiriwa hospitalini -pia katika hospitali ya Sion – walizaliwa kwa njia ya upasuaji, huku waliosalia wakizaliwa kwa njia ya kawaida, walisema maafisa.

Hamsini na sita kati yao walikua ni wa kiume, huku 59 wakiwa ni wa kike. Ishirini na wawili kati ya wakinamama hawa waliletwa kutoka katika hospitali nyingine : Haijawa wazi ikiwa wengi wa wanawake hawa walipata maambukizi nyumbani, sehemu nyingine au hospitalini.

Timu ya madaktari 65 na wauguzi 24 wamekua wakiwatibu wanawake walioambukizwa corona katika vitanda 40 maalumu. Huku kukiwa na idadi kubwa ya maambukizi , hospitali inapanga kuongeza vitanda vingine 34 kwa ajili ya wanawake wajawazito wenye maambukizi ya Covid-19.

Wanawake hao walijifungulia kwenye vitanda 6 vya kujifungulia katika vyumba vitatu vya upasuaji na wauguzi na madaktari wa nusu kaputi wanatumia mavazi ya kujikinga dhidi ya maambukizi ya corona.

“Tunabahati kuwa wengi miongoni mwa wanawake waliopatwa na maambukizi kwa sasa hawaonyeshi dalili yoyote kabisa ya virusi vya corona. Baadhi yao walikua na homa na waliripoti kukosa pumzi. Tumewatibu na kuwaruhusu waende nyumbani baada ya kujifungua ,” Dr Arun Nayak, mkuu wa kitengo cha wanawake katika hospitali, amesema

staff at sion hospital
Madaktari katika hospitali wamewazalizsha zaidi ya watoto 100 kutoka kwa akinamama wenye virusi vya corona

” Kuna wasiwasi mkubwa miongoni mwa wanawake hawa . Wanatuambia kila mara kwamba wanaweza kufa lakini tunapaswa kuhakikisha kuwa watoto wao ni wenye afya.”

Baada ya kujifungua, wakinamama wanabaki katika wodi maalumu iliyotenga kwa ajili ya wagonjwa wa Covid-19 kwa wiki na kupewa dawa ya Hydroxychloroquine. Baada ya kukaa karantini kwa muda wa siku 10 katika kituo tofauti. Watoto hawajatengwa na wananyonyeshwa na mama zao huku wakiwa wamevaa barakoa

Mwezi Februari, mtoto mchanga wa Kichina alipatikana na virusi vya corona saa 30 tu baada ya kuzaliwa katika Wuhan , kitovu cha virusi.

Na Mwezi Machi mtoto aliyepatikana na maambukizi alikufa katika mji wa Chicago – akiwa ni kifo cha kwanza cha mtoto aliye chini ya umri wa mwaka mmoja aliyeambukia virusi vya corona nchini Marekani. Mtoto mwenye umri wa miezi sita alikufa kutokana na matatizo yanayohusiana na Covid-19 Connecticut. Na mapema mwezi huu, mtoto wa siku tatu alikufa baada ya mama yake kupatikana virusi vya corona katika Wales.

Maambukizi ya mama kwa mtoto ya virusi vya corona- tumboni au wakati wa kujifungua, kabla ya mtoto kufikiwa na majimaji ya mfumo wa kupumua wa mama yake- ni ya nadra , Dkt Adam Ratner, mkurugenzi wa watoto kitengo cha magonjwa yanayoambukizwa katika hospitali ya watoto ya Chuo Kikuu cha tiba – cha New York School of Medicine and Hassenfeld Children’s Hospital at NYU Langone Health, aliiambia BBC.

Hii bilashaka kwa ongezeko la visa vya aina hii ” hali inabadilika haraka na data mpya idadi inaweza kupanda “.

Dokta Ratner anasema kuna data zinazojitokeza ambazo zinaonyesha kuwa virusi vya corona vinaweza kuonekana katika nyama ya kondo la nyuma la uzazi(placenta)

Pia kumekua na ripoti za watoto wachanga wanaokufa wakati wakiwa bado vijusi ndai ya mwanamke mjamzito kutokana na maambukizi makali, alisema, “lakini hiyo inaweza kuwa ni kwasababu nyingine tofauti na maambukizi ya moja kwa moja ya kijusi “.

mother at sion hospital
Hospitali ina kitengo maalumu cha akinamama walioambukizwa Covid-19

Dkt Ratner alisema kuwa hakuna na ripoti ya “kinga ya mwili kukataa kufanyakazi ” katika watoto wanaozaliwa ambayo inaweza “kuzuwia maambukizi katika mfuko wa uzazi au wakati wa kuzaliwa kwa mtoto”. Hiyo inamaanisha kuwa mtoto anaweza kuwa aliambukizwa akiwa tumboni..

“Ni muhimu sana kuendelea kuchunguza maswali haya na kuangalia matokeo ya watoto wanaozaliwa na Covid-19, hata kama hawakupata maambukizi wakiwatumboni ,” Dkt Ratner alisema.

Dkt Ratner alisema alisaidia kuwahudumia watoto wachanga kadhaa wa wakinamama wenye maambukizi katika hospitali yake.

” Tumewaruhusu kuwanyonyesha maziwa ambayo yamekamuliwa kutoka kwa mama zaona tunajaribu kutafuta mpango wa kuwakinga watoto kupata virusi wakiwa wadogo.

” Watoto wadogo sana ambao nimekwishawaona kwa ujumla wamefanya vizuri ,”alisema.

Katika hospitali ya Mumbai, idadi ya watoto wachanga wanaozaliwa kwa akinamama wenye Covid-19 wamekua zaidi kidogo ya 20% ya jumla ya watoto wanaozaliwa katika kipindi hicho hicho.

“Wakati mmoja tulihisi tumekasirika baada ya mama mwenye umri wa miaka 28 ambaye alikufa wiki iliyopita kwa virusi vya corona baada ya kujifungua mtoto wa kiume. Ini lake liliathirika na alikufa haraka ,” Dkt Nayak aliiambia BBC

“Aligundua jinsi tulivyoshindwa kumpa msaada wakati wa matibabu. Aliuliza mara kwa mara, bila kujua afanye nini , ‘ Kuna chochote kinaweza kufanyika?'”

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents