Burudani

Iggy Azalea aamua kujiondoa kwenye mitandao ya kijamii kufuatia beef za Twitter

Rapper wa kike mwenye asili ya Australia, Iggy Azalea ametangaza kujipumzisha nje ya mitandao ya kijamii kufuatia beef na maoni hasi kuhusu yeye ambayo amekuwa akipokea kila mara mtandaoni hasa kupitia Twitter.

Iggy A

“But I also want to let my fans know iam taking some time away from social media. I need to be happy and it is too negative and draining.” Alitweet.

Kufuatia uamuzi huo Iggy amesema kuwa uongozi wake ndio utasimamia akaunti zake za mitandao ya kijamii kuanzia sasa kwaajili ya kutoa maendeleo ya kazi zake.

“My management will tweet/run my accounts from today onwards…Peace out!”

Katika tweet nyingi alizoandika kuelezea sababu za kujiondoa kwenye mitandao ya kijamii, Iggy amesema kuwa chuki anazoziona mtandaoni dhidi yake zinamfanya awe mtu mwenye hasira huku hapendi kuwa hivyo.

“I feel the hatred and pettiness I see online at all times is making me become an angry person and I cannot be that.”

Miongoni mwa mastaa ambao amekuwa na beef nao kupitia mitandao ya kijamii ni pamoja na
Azealia Banks, Jill Scott, Eve na Snoop Dogg.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents