Burudani

Iggy Azalea ataja siku atakayoachia albamu ya ‘Digital Distortion’

Iggy Azalea amefunguka muda atakaoachia albamu yake mpya ya ‘Digital Distortion’ ambayo imekuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu.

Akiongea katika kipindi cha Zach Sang Show, rapper huyo kutoka Australia amesema albamu yake hiyo ya pili itatoka Juni 30 ya mwaka huu kama pre order lakini mwezi Julai itakuwa inapatikana sehemu zote.

Katika albamu hiyo Iggy amewashiikisha wasanii kama YG, French Montana na Lil Uzi Vert. Wakati huo huo imetayarishwa na maproducer kibao akiwemo Chordz, Nezzo, Omega, Ryan Avilez, Louis Harden, Zedd na wengine.

Wimbo wa kwanza ambao utapatikana katika albamu hiyo ni ‘Team’ ambao aliuachia Machi mwaka jana.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents