IGP aahidi usalama na utulivu

Inspekta Generali wa polisi Tanzania,Said Mwema amewahakikishia wananchi amani na utulivu kwa kipindi hiki cha uchaguzi.

JESHI LA POLISI limejipanga vizuri ili kuhakikisha Uchaguzi Mkuu unakuwa wa huru na haki kwa kuzingatia sheria ya uchaguzi, kanuni na taratibu zilizowekwa na Tume ya Taifa Uchaguzi(NEC) zinafuatwa na kutekelezwa pasipo uvunjifu wa wowote wa sheria.

Aidha jeshi hilo limesema kwamba kampeni litahakikisha mikutano ya kampeni itafanyika na kumalizika katika eneo kwa muda uliopangwa, pia vifaa vya kupigia kura kuwa kwenye hali ya usalama na wagombea wote wa nafasi za uongozi, likiwemo suala zima la kukabiliana na vitendo vingine vya uhalifu.

Hayo yalisemwa na Inspekta Mkuu wa Jeshi la Polisi( IGP), Said Mwema, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, ambapo ameiasa jamii kulinda amani hasa kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa rais, wabunge na madiwani unaotarajiwa kufanyika Octoba mwaka huu.

“Sheria haina udhuru mtu akitenda kosa, sheria haitamfumbia macho itachukua mkondo wake. Tutumie nafasi hii vema katika kutimiza haki na wajibu wetu kushirikiana ili kuhakikisha zoezi zima la kampeni na kupiga kura linakwenda kwa amani , usalama utulivu bila viashiria vyovyote vya vurugu,” alisema Mwema.

Aliwakumbusha pia wagombea juu ya kuhakikisha wanaheshimu sheria za nchi kwani kwa yeyote atakayekiuka itachukua mkondo wake ili kuhakikisha zoezi linakwenda kwa amani.

“Jeshi litafanya kazi bila upendeleo wowote kwa chombo cha siasa” aliongeza Mwema.

Naye Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba akielezea juu ya uwezekano wa kutokea kwa matukio ya kigaidi wakati wa uchaguzi alisema kuwa ugaidi ni tatizo la dunia nzima, hivyo nchi za Afrika Mashariki zimejiandaa vizuri kukabiliana nalo.

Alisema miongoni mwa jitihada zinazofanyika ni kupanga mikakati ya pamoja na pia askari wanaendelea na mafunzo maalum juu ya kupambana na tatizo hilo.Mwema aliyasema hayo baada ya Uchaguzi kuanza rasmi jana ambapo wagombea takriban 9 wa vyama mbalimbali walirejesha fomu za kugombea nafasi ya Urais,na shughuli za kampeni kuzinduliwa.

Uchaguzi mkuu utafanyika Oktoba 31 mwaka huu.

Mungu Ibariki Tanzania.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents