Siasa

IGP Simon Sirro: Jeshi la Polisi halijihusishi na siasa, viongozi wa siasa watimize wajibu wao (+Video)

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini  IGP Simon Sirro, amewahimiza askari wa Jeshi hilo kutimiza wajibu wao kwa kuhakikisha wanatenda haki  na kufuata taratibu zilizopo.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini  IGP Simon Sirro

Akizungumza na waandishi wa habari  hii leo Oktoba 20,2020,visiwani Zanzibar amesema kazi ya jeshi la polisi ni kuhakikisha wanasimamia sheria na watanzania wanafanya uchaguzi kwa amani ambapo pia amewataka wadau wa uchaguzi kutimiza wajibu wao ipasavyo bila kuvunja sheria.

“Tume ya uchaguzi itimize wajibu wao,viongozi wa siasa watimize wajibu wao na kubwa zaidi nazungumzia hili la kusema kuna baadhi ya kikundi cha watu wamesema watatangaza matokeo hiyo imenishangaza kidogo’’, amesema IGP Sirro.

IGP Sirro ameongeza kuwa viongozi wa siasa wanatakiwa kufuata sheria ambapo pia amewakumbusha kwamba wenye mamlaka ya kutangaza matokeo ni NEC na ZEC na si mtu mwingine yoyote.

https://www.instagram.com/tv/CGmKYcHBcLk/

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents