Habari

IGP Sirro aeleza yanayoendelea Mtwara

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Sirro amesema Jeshi la Polisi litachukua muda mfupi kukabiliana na uhalifu unaoendelea katika Mkoa wa Mtwara, kama ilivyofanya katika kukabiliana na mauaji ya raia katika Wilaya za Kibiti, Rufiji na Mkuranga mkoani Pwani.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Sirro.

IGP Sirro amesema hayo wakati akizungumza na wakazi wa Kitava mkoani humo, ambapo ameahidi kuwa tatizo hilo halitachukua muda mrefu kwani vyombo vya ulinzi na usalama vimejipanga kutokomeza uhalifu huo waliohusika na matukio ya utesaji raia na uharibifu wa mali zao wanachukuliwa hatua.

“Wananchi wetu wamepata shida na waliofanya shida lazima washughulikiwe kwa mujibu wa sheria zetu kwa kushirikiana na Msumbiji sababu wana taarifa watu wanaotoka huko kuja kufanya Tanzania,” amesema IGP Sirro.

IGP Sirro ameongeza kuwa, “Kimsingi ni kwamba, tumejipanga vizuri wananchi wetu waendelee kurudi kwenye yale maeneo waliyokimbia kule mpakani (mpakani mwa Tanzania na Msumbiji), tumeshajiimarisha, tutahakikisha hili tatizo litachukua muda mfupi kama ilivyokua kwenye tatizo la Kibiti na Ikwiriri ilivyochukua muda mfupi. Hawa wahalifu tutawashughulikia huko huko.”

Chanzo Eatv

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents