Habari

IGP Sirro awataka askari kufanya kazi kwa weledi

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, amewataka askari wa Jeshi hilo kufanyakazi kwa weledi na kwa kuzingatia sheria na taratibu zitakazosaidia kujenga taswira chanya hasa wanapotekeleza majukumu yao ya kila siku.

IGP Sirro ameyasema hayo alipokutana na kuzungumza na askari na maofisa wa mkoa wa Kagera, wakati akiwa kwenye muendelezo wa ziara zake zenye lengo la kujitambulisha pamoja na kujua changamoto wanazokutananazo wakati wakitekeleza majukumu yao.

Alisema kuwa, kila askari analojukumu mbele yake la kuhakikisha suala la uhalifu na wahalifu linadhibitiwa hususan kwa kuimarisha usalama wa raia na mali zao huku wakizingatia kuwa, mkoa huo unapakana na nchi jirani za Uganda, Rwanda na Burundi.

Hata hivyo, katika ziara yake, IGP Sirro, amewahakikishia askari na maofisa kuwa, yupo tayari kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza na kuwataka askari kuongeza kasi ya kukabiliana na matishio ya kiuhalifu na wahalifu ili kuifanya jamii kuishi kwa amani na utulivu.

Aidha, katika ziara hiyo, masuala mbalimbali yamejadiliwa huku mbinu mpya za kukabiliana na uhalifu katika mkoa huo pamoja na wilaya zake zikiibuliwa kwa kuzingatia kuimarisha usalama wa raia na mali zao.

Taarifa na Jeshi la Polisi

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents