Habari

IGP Sirro awatuliza Wananchi, wakiri kupokea taarifa kuhusu tahadhari ya shambulio kutokea Dar

Usiku wa Jumatano (Juni 20 ) Ubalozi wa Marekani Tanzania ulitoa taarifa kwamba kuna tetesi za kutokea kwa shambulio katika maeneo ya Masaki jijini Dar hususani katika migahawa na hoteli ya Slipway Shopping Center ya Msasani, taarifa ambayo iliibua wasiwasi mkiubwa kwa wakazi wa maeno hayo.

Jeshi la Polisi nchini Tanzania limewatoa hofu wananchi juu ya tishio la ugaidi katika maeneo ya Masaki jijini Dar es Salaam, likisema taarifa hizo zimeshaanza kufanyiwa kazi.

Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) nchini Tanzania, Simon Sirro ameiambia Mwananchi usiku huu Juni 18, 2019 kuwa jeshi lake lilishapata fununu za shambulio hilo kabla Ubalozi wa Marekani kutoa tahadhari juu ya tukio hilo kupitia tovuti yake Juni 18, 2019.

Akizungumzia taarifa hiyo ya Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, IGP Sirro amesema, “hiyo ni taarifa kama taarifa nyingine, inaweza kuwa ya kweli au uongo, lakini sisi kama vyombo vya ulinzi huwa hatupuuzi jambo. Tangu jana (Jumanne Juni 17, 2019) tulipata hiyo taarifa kwa hiyo tuko vizuri, timu zetu za operesheni na intelijensia na wengine tunaifanyia kazi.”

Katika tangazo lake Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania inaeleza kuwapo kwa uvumi wa kutokea kwa shambulio la kigaidi katika eneo la Masaki hususan hoteli za kitalii na maduka ya maeneo hayo ya ufukwe wa Bahari ya Hindi.

Ubalozi huo umewataka wakazi kuwa makini na maeneo hayo, kujiepusha na makundi na kufuatilia taarifa kupitia vyombo vya habari.

https://www.instagram.com/p/By6v3-WBo0X/

Baada ya uvumi huo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda aliibuka usiku huo na kukanusha kwamba hauna taarifa kama hiyo huku akiwataka wananchi kuacha kusambaza taarifa ambazo hazijathibitishwa.

Kutokana na taarifa hizo, wananchi wamekuwa na maoni tofauti huku wakiitaka serikali kuchukua tahadhari zaidi. Haya ni baadhi ya maoni kutoka mitandaoni.

John Wambura
Hii si ya kupuuza,maana vyombo vyetu vya usalama viko bize na chadema,,hao jamaa wako juu ki intelejensia..tuchukue tahadhari ndugu.

Thebestfetty
Nimewaza lakini . Kama taarifa zipo muda mrefu na zinafanyiwa kazi KWANINI UBALOZI WA MAREKANI NCHINI waamue kutoa taarifa hii na je ni sawa wao kutoa taarifa kabla ya Vyonbo vyetu vya usalama. Kama sio sawa kwanini wafanye hivyo ? Kama tahadhari hii tunayo na tunaifanyia kazi je haikupaswa kujulishwa wananchi atleast kwa ONYO (tusiwe katika mikusanyiko naeneo tajwa) kama walivyofanya ubalozi wa Marekani??? Je tunahaki ya kupewa hizi taarifa na vyombo vyetu vya usalama??? Hebu tuongee maana nimeshaangaa tu. AU KUNA YALIYOFICHIKA HAPA??? NIKO HOVES.

leostonchisanza
Marekani huwa wanatoa tahadhari kwa raia wake popote walipo duniani wakiona Kuna tetesi za mashambulio.

ekk2018
Thanks so much for the information @usembassytz With this information you will not only save the Americans but us also.


Simon_jilala

Wamarekani wametoa tahadhari ya kuwatahadharisha Wamarekani wanaoishi maeneo hayo au Tz. Na wao wana uwezo mkubwa mno katika mambo ya Ulinzi na Usalama.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents