Burudani

Ijue ngoma nyingine ya Star aliyoandika Barnaba, bado ipo kwenye chart

Msanii wa Bongo Flava, Peter Msechu ameweka wazi kuwa wimbo wake mpya ‘Pakawa’ imeandikiwa na Barnaba.

 

Peter Msechu aliwahi kutangaza kuwa yeye anapokea nyimbo kutoka kwa wasanii na waandishi kitu ambacho anakiri kwa sasa amekuwa akipokea nyimbo nyingi zaidi kwa wastani wa tano au sita kwa siku.

“Wimbo wa Pakawa umeandikwa na Barnaba alinitukuu, tulikaa kwa muda mrefu sana bila kuutoa, alikuwa akinisihii achia huo wimbo lakini sikuweza kuuachia lakini nafikiri ni moja ya kitu kinaweza kuja kuwa kikubwa sana,” ameiambia Planet Bongo ya EA Radio.

Msanii Barnaba ameshawahi kuwaandikia nyimbo wasanii mbali mbali kamaVanessa Mdee, Lulu Diva, Linah na wengine kibao kutoka THT.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents