Habari

Ikiwa ni siku ya Wanawake duniani, Shirika la ndege ya Ethiopia limewaachia marubani wa kike kurusha ndege kwenda Norway

Shirika la Ndege la Ethiopia linaadhimisha siku ya kimataifa ya wanawake duniani kwa kuwaacha wafanyakazi wanawake pekee kurusha ndege kutoka Addis Ababa mpaka Oslo. Shirika hilo lilitangaza kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa ”wanawake watajidai kwenye anga kwa mara ya tano, wakiruka kuelekea Oslo tarehe 8 mwezi Machi”

Kwa mujibu wa BBC. Ndege hiyo itawahusisha wanawake pekee nje ya ndege na ndani ya ndege, iliandikwa pia kwenye ukurasa wa Facebook.

Hii inamaanisha kuwa huduma za uwanja wa ndege,udhibiti mizigo,wanaotazama ndege zinapopaki, mipango ya ndani ya ndege, ulinzi na usalama pia huduma za chakula

Mkuu wa shirika hilo Tewolde Gabre Mariam alieleza kuwa hatua hii ni kusheherekea wanawake barani Afrika ambako ”usawa wa kijinsia bado unakabiliwa na changamoto”.

Shirika hilo limesema lina matumaini kuwa litasaidia kuonyesha”nguvu ya mwanamke duniani”

‘Tunayo furaha kubwa kwa kuwa tuna wanawake wabunifu katika kila nyanja kwenye masuala ya anga,” alieleza

”Wanawake ni sehemu ya hadithi yetu ya mafanikio tangu awali, na kwa siku hii tunatambua mchango wao kwa shirika na kwa soko la masuala ya anga, nchi yetu na bara zima kwa ujumla.”

Hii si mara ya kwanza kwa shirika hili kubwa Afrika, Kabla yake wanawake walishafanya safari kwenda Bangkok, Kigali, Lagos na Buenos Aires.

”Wanawake ni sehemu ya hadithi yetu ya mafanikio tangu awali, na kwa siku hii tunatambua mchango wao kwa shirika na kwa soko la masuala ya anga, nchi yetu na bara zima kwa ujumla.”

Hii si mara ya kwanza kwa shirika hili kubwa Afrika, Kabla yake wanawake walishafanya safari kwenda Bangkok, Kigali, Lagos na Buenos Aires.

Katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani mwaka jana, Shirika la Ndege la India ,lilikua shirika la kwanza kuruka duniani kote likiwa na wanawake watupu ndani ya ndege hiyo. Wanawake walifanya kazi katika idara zote nane.

Pia British Airways mwaka jana wanawake zaidi ya 60 walitoa huduma ya safari kwa ndege yao kubwa nchini Uingereza wakiirusha kutoka London Heathrow kwenda Glasgow.

Sauti za wanawake kwenye chumba cha rubani

Shirika la Ndege la Ethiopia limeonyesha mchango wa muda mrefu wa wanawake katika sekta hiyo na mafanikio waliyoyapata katika eneo hili ambalo kwa kiasi kikubwa limetawaliwa na wanaume hasa katika upande wa marubani na wahandisi wa ndege.

Dokta Saba Fikru, mkuu wa kitengo cha dawa na huduma za afya ndani ya ndege amesema asilimia 35 ya wafanyakazi 16,000 wa Kampuni ni wanawake.

”Sasa hivi idadi nyingine inaongezeka kwani wanawake wanamalizia mafunzo ya urubani.Sasa tunaweza kusikia sauti za wanawake zikitoka kwenye chumba cha rubani.”Alieleza.

By Ally Juma.


Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents