Habari

iKnife: Kisu chenye uwezo wa kugundua kama sehemu inayokatwa ina Kansa wakati wa operation (video)

Wanasayansi wametengeneza kisu cha upasuaji ‘intelligent surgical knife’ chenye uwezo wa kugundua kwa sekunde kama sehemu inayokatwa katika mwili wa binadamu wakati wa upasuaji ina kansa ama laa.

Kisu hicho kilichobuniwa na watafiti wa Imperial College huko London, Uingereza kitawawezesha madaktati kufanya upasuaji wenye uhakika zaidi kwa wagonjwa wao.

Kwa mujibu wa wataalam upasuaji mara nyingi huwa ni vigumu kujua kwa kuona mwisho wa uvimbe hivyo ni ngumu kwa surgeon kufahamu mahali anapotakiwa kuishia kukata, hivyo wakati mwingine cell za kansa huachwa bila kuondolewa na kuhitaji upasuaji mwingine kwa mgojwa baadaye.

Kisu hicho kipya kilichopewa jina la “iknife” yaani (Intelligent Knife) kimetengenezwa kukabiliana na tatizo kama hilo na katika majaribio ya kwanza yaliyofanywa, kilitoa majibu sahihi kwa wagonjwa 91 kwa mujibu wa watafiti wa Imperial College London waliotoa ripoti yao Jumatano wiki hii.

Mgunduzi wa kifaa hicho Zoltan Takats wa Imperial College alisema malengo yake yalikuwa ni kufanya majaribio kwa wagonjwa kati ya 1000 mpaka 1500 wanaosumbuliwa na aina tofauti za kansa, na mchakato huo wa majaribio unategewa kuchukua kati ya miaka 2 au 3 kabla iknife haijawasilishwa kwa mamlaka zinazohusika kupitisha iingie katika biashara.

Video:AlJazeera

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents