Burudani ya Michezo Live

Ili wasanii wa Bongo wapate deal za record label kubwa duniani wafanyeje? KBC wa Kwanza Unit analo jibu

Leo tumeandika makala isemayo: Ni muda sasa wa Tanzania kuwa na record labels za uhakika ambayo imemvutia aliyewahi kuwa member wa kundi la Kwanza Unit, Kibacha aka KBC ambaye pia aliwahi kuwa mtangazaji wa Clouds FM.

page

KBC ameeleza kwa ufupi ni mambo gani ya kuzingatia ili wasanii wa Tanzania waanze kupata mashavu kwenye record label kubwa duniani:

“LABELS kubwa za kimataifa zimeanza kuangazia macho yake Afrika, mfano SONY Africa, ambao walim-sign mwanadada XTATIC wa Kenya. Lakini kwa hizi label kuja hapa kwetu mabadiliko mengi lazima yafanyike. Cha kwanza ni QUALITY and CREATIVITY in our music. Wasanii na Maproducer wa Tanzania inabidi wabadilike. Tufunguke kimawazo katika fani na biashara hii ya muziki. Inabidi tuepukane na UVIVU katika Production na Utunzi, kwa kusingizia msemo wa “Kibongo-Bongo”.

Labels kubwa zinatafuta muziki utakaokubalika dunia nzima.. Vile vile swala la HATI MILIKI linabidi lirekebishwe. Mfumo wa Usambazaji wa kazi za kisanii inabidi ubadilike. Record Label ni biashara. Ni rahisi kwa Label kama Sony ku sign artist kama PROF JAY kama kuna uhakika mashabiki wake wote wa East africa watanunua CD yake.

Sasa tuangalie population ya East Africa, 131.1 million people in 2010. So let’s assume half of the population are the Bongo Flava listeners who are willing to buy records, bila ya kufanya uharamia wa copy haramu, Label itaweza kuuza 14,730,379.5 RECORDS, 2,000,000 or more units: Multi-Platinum album, 10,000,000 units: Diamond album. Kwa mfano kila santuri ikiuuzwa £5..Label ingetengeneza pesa ngapi? wadau na wahasibu nawaachia mmalizie haya mahesabu. Lakini naomba tusisahau kupiga hesabu ni kiasi gani serikali italipwa TAX kutokana na mauzo hayo? Labda itawaonyesha THAMANI ya wasanii wetu na kazi zao.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW