Burudani

Ilifika hatua msanii akiambiwa katekwa anaona ndio kiki – Nikki Mbishi

Msanii wa muziki wa hip hop Bongo, Nikki Mbishi amesema katika muziki huo  kuna wasanii wanaendekeza sana kiki kuliko muziki wao.

Rapper huyo ameiambia The Playlist ya Times Fm kuwa kitendo hicho is kizuri katika muziki na amekuwa akikemea katika ngoma zake.

“Kuna wakati ulifikia sijui bado upo au unaendelea matukio ya kisiasa yalikuwa yanafunika hata muziki mtu unatoa ngoma yako watu wanataka kusikia mambo yako mengine,” amesema Nikki Mbishi.

“Ilifika hatua hiyo wasanii wengi wakawa mtu akiambia katekwa anaona ndio kiki, inaonekana ndio dili, kwa hiyo kila mtu ndio anajifanya kama kapotea, katekwa mara sijui kahusishwa na vitu gani na serikali ilimradi iwe hivyo,” ameongeza.

Nikki Mbishi kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la Nimekumiss.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents