Habari

Imam Mkuu Ghana asherehekea siku ya kuzaliwa kwa kuhudhuria misa ya kanisa katoliki

Imam mkuu nchini Ghana ni mtu wa maneno machache lakini kiongozi huyo wa dini mwenye umri wa miaka 100 ana uwezo wa kuwaleta watu pamoja. Aliamua kusherehekia siku yake ya kuzaliwa kwa kuhudhuria misa ya kanisa katoliki.

 

Sheikh Osman Sharubutu (C), in green, sitting in a pew at the Christ the King Catholic Church in Accra, Ghana

Picha za Sheikh Osman Sharubutu, akiwa ameketi katikati ya waumini wa Kikristo katika kanisa katoliki la Christ the King Catholic mjini Accra wakati wa ibada ya pasaka imezua gumzo katika mitandao ya kijamii.

Mufti huyo mkuu wa Ghana anawaakilisha waumini wa dini ya Kiislamu waliyo wachache, anataka kuhakikisha ameacha utawala wa amani katika uongozi wake – kama sehemu ya kuleta jamii pamoja bila kujali misingi yao ya kidini.

Mufti huyo mkuu wa Ghana anawaakilisha waumini wa dini ya Kiislamu waliyo wachache, anataka kuhakikisha ameacha utawala wa amani katika uongozi wake – kama sehemu ya kuleta jamii pamoja bila kujali misingi yao ya kidini

Hatua yake ya kuingia kanisani ilishabihiana na kisa cha makanisa kushambuliwa kwa mabomu na watu wanaodaiwa kuwa wanamgambo wa Kiislam nchini Sri Lanka, ambapo watu zaidi ya 250 waliuawa makanisani na katika Hoteli za kifahari.

Wale wanaounga mkono hatua ya imam huyo walimtaja kama nuru inayoangaza gizani.

https://citinewsroom.com/2019/04/21/chief-imam-worships-with-christ-the-king-church-ahead-of-100th-birthday-celebration/?fbclid=IwAR2SRRFOfVkN5O3wIGXT3sGkju8yhPHp7TfYE2U2MaSIZNdTIA2ZLpFYHxs

Sio kila mtu aliyefurahishwa na hatua ya Sheikh Osman Sharubutu – wengine walisema ni laana, kwa muislamu kushiriki sala ya kikristo.

Lakini Sheikh Sharubutu anasisitiza kuwa hakuwa anashiriki maombi bali hatua yake ilikuwa ya kuimarisha uhusiano kati ya Waislamu na Wakriristo.

“Kiongozi huyu anajaribu kubadilisha dhana potovu kuhusiana na dini ya Kiislamu, kwamba ni dini inayochukia dini zingine,” msemaji wake Aremeyao Shaibu aliiambia BBC.

Presentational grey line

Mchungaji aliyekuwa rafiki wa Imam

Taarifa ya Elizabeth Ohene, AccraFather Andrew Campbell (L) and Sheikh Osman Sharubutu (R)

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Tofauti na Imam mkuu wa imam Ghana, Father Andrew Campbell, kasisi wa parokia ya kanisa la Christ the King Catholic, yeye sio mtu wa maneno machache.

Father Andrew wa miaka 73 alizaliwa Ireland na alifika Ghana mwaka 1971 kufanya kazi kama mmishonari.

Kwa zidi ya miaka 48 amekuwa balozi wa kazi ambazo hazikupendelewa na watu wengi ilikukabiliana na ubaguzi wa kidini.

Kiongoz huyo amwkuwaakisaidia baadhi ya miradi na sera za serikali, lakini pia hakusita kupaza sauti serikali inapoenda kinyume na matarajio yake.

Amepewa uraia wa Ghana lakini amekataa kuunga mkono mienendo ya watu wa taifa hilo la kutofika katika hafla walizoalikwa kwa muda uliyowekwa.

Lakini hatua yake ya kushirikiana na kiongozi wa dini ya Kiislam imetajwa kuwa ya kipekee na ambayo haikutarajiwa.

Sheikh Sharubutu, amekuwa kiongozi wa ngazi ya juu wa dini ya Kiislam nchini Ghana kwa miaka 26 years, na wakati wote amekuwa akisisitiza kuwa dini hiyo imejengwa katika msingi wa amani na upendo kama ilivyobainika katika hotuba yake ya kila siku ya Ijumaa katika msikiti mkuu jijini Accra

Makaazi yake ni wazi kwa majirani zake ambao wengi wanatoka katika jamii masikini

Kwa miaka kadhaa sasa mamia ya watu huja kwakle kuteka maji kila asubuhi huku wengine wakipewa chakula bila malipo.

Waumini wa dini ya Kiislam nchini Ghana, ni 18% ya idadi ya watu wote nchini humo na taifa hilo halina historia ya mzozo wa kidini.

Lakini wakati mwingine hali ya taharuki iikizuka kiongozi huyo huwa mstari wa mbele kutafuta ufumbuzi wa haraka. Yeye nmi mwanachama wa baraza la kitaifa la Amani,ambalo linajumuisha viongozi 13 hususan wa kidini.

Mzozo wa ardhi ya makaburi

Mapema mwaka huu, aliwatuliza vijana wa kundi la kiislam waliovamia kanisa moja jijini Accra baada ya mchungaji wa kanisa hilo kutabiri atafarika katika kipindi cha miezi 12 ijayo.

Aliwasihi vijana hao waliyokua wamejihamii kwa mapanga kumsamehea mchungaji huyo hatua ambayo ilimfanya mkuu wa polisi katika eneo hilo kumshukuru.

Wakati hali ya hatari ilipowekwa katika barabara za Old Tafo mjini Kumasi kufuatia mzozo wa ardhi ya makaburi mwaka 2016, aliingilia kati na kutulizi hali iliyopelekea amri hiyo.

People pray during the celebration of the Eid al-Fitr at Independence Square in Accra, Ghana - June 2017

Waumini wa dini ya Kiislam nchini Ghana, ni 18% ya idadi ya watu wote nchini humo

Rekodi ya Sheikh Sharubutu ya miaka 100:

  • Amefungisha ndoa zaidi ya 5,000
  • Ameongoza ibada ya mazishi zaidi ya 4,000
  • Ameongoza hafla ya sherehe ya kuwapatia watoto majina zaidi ya mara10,000

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents