Habari

Imeelezwa ajali ya magari mawili iliyoua watu zaidi ya 50 nchini Ghana, chanzo ni dereva wa moja ya magari hayo alikuwa akisinzia

Takribani watu 60 wameuawa siku ya Ijumaa baada ya mabasi mawili kugongana katika eneo la Kitampo Kusini mwa Ghana. Kwa mujibu wa polisi ajali hiyo ilitokea usiku wa kuamkia leo katika mkoa wa Bono Mashariki.

Kwa mujibu wa DW. Kamamda wa polisi Antwi Gyawu ameliambia  shirika la habari la AFP kwamba magari hayo yalikuwa yakitokea pande tofauti wakati ajali hiyo ilipotokea. Kamanda Gyawu amesema katika ajali hiyo iliyoua wato 60 moja ya mabasi hayo lilishika moto huku jingine likiharibiwa vibaya.

Mabasi hayo yanakadiriwa kuwa yalikuwa yamebeba 50 kila moja. Watoa huduma za dharura waliwasili katika eneo la tukio ikiwa ni pamoja na vikosi vya kuzima moto ili kuzima moto uliolipuka kutokana na ajali hiyo. Daktari Kwame Arhin katika wa Hospitali ya serikali ya Kitampo amesema watu 28 wamefikishwa hospitalini hapo kutokana na majeraha.

Dk. Arhin ameliambia shirika la habari la AFP kuwa watu 7 kati ya 28 waliofikishwa hospitalini hapo wako kwenye hali mbaya na wengi wamepata majeraha makubwa vichwani, na pia miili ya watu kadhaa waliofariki kwenye ajali hiyo imehifadhiwa Hospitalini hapo.

Uchunguzi wa ajali waendelea

Ingawa chanzo cha ajali hiyo bado kinachunguzwa, vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa mmoja wa madereva wa mabasi hayo alishindwa kulidhibiti basi kutokana na kuzidiwa na usingizi. Kamanda wa kikosi cha zimamoto wa eneo la Kitampo kulikotokea ajali hiyo Ankomah Twene, amesema abiria walionusurika wamewaambia kuwa dereva wao alikuwa akisinzia lakini abiria hao walipomsihi aweke gari kando kupumzika alikataa. Kamanda Twene anasema huenda hilo ndilo lililochangia kutokea kwa ajali hiyo.

Ghana Busunglück 71 Tote (picture-alliance/dpa)

Moja ya ajali ya basi eneo la Kintampo Februari, 2016

Mmoja wa walionusurika na ajali hiyo Rose Anane amesema ”Nilikuwa nimelala kisha nikasikia kishindo kikubwa. Tulifanikiwa kuvunja kioo na ni baadhi yetu tu, kama watu kumi hivi ndio tuliofanikiwa kujiokoa. Ndani ya dakika kadhaa basi likashika moto watu wengine wakiwa wamenasa.”

Ajali hiyo imeibua upya wito kwa mamlaka husika nchini humo kuhakikisha kuwa watu wanatii sheria za barabarani ili kupunguza vifo na majeraha yanayotokana na barabara mbovu nchini humo. Mkazi wa eneo ilipotokea ajali hiyo Gifty Mintah amesema pamoja na kutoa malalamiko katika mikutano kuhusu kuwekamatuta katika barabara hiyo. Ajali zimekuwa zikitokea mara kwa mara nchini Ghana,kutokana na kutofanyiwa marekebisho ipasavyo, kupuuzwa kwa sheria za barabarani pamoja na magari mabovu.

 Kwa mujibu wa Idara ya Polisi ya usimamizi wa  usafirishaji nchini Ghana, wastani wa watu sita hufariki dunia kila siku kutokana na ajali za barabarani. Mwezi Februari mwaka 2016, watu 70 walikufa na 13 kujeruhiwa baada ya mabasi mawili kugongana uso kwa uso katika mji huo huo wa Kitampo. Mwezi Julai mwaka 2017 mmoja wa wachezaji wa klabu kubwa nchini humo ya Asante Kotoko alijeruhiwa baada ya basi lililokuwa limewabeba wachezaji wa timu hiyo kupata ajali.

By Ally Juma.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents