Habari

IMF yaunga mkono jitihada za Rais Magufuli

Shirika la Fedha Duniani (IMF), limeunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli za kupambana na vitendo vya rushwa na ukwepaji na kusema kuwa hatua hiyo kielelezo cha dhamira ya kweli ya Serikali yake ya kuleta maendeleo kwa faida ya wananchi wote.

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Dk. Tao Zhang amesema mjini Dar es Salaam leo kuwa Tanzania ni moja kati ya nchi zinazofanya vizuri katika kukuza uchumi wake.

“Kuna mambo mengi ambayo yanatoa fursa kwenu ikiwemo uanachama wenu katika katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, rasilimali ambazo zimo mbioni kupatikana katika miaka ya karibuni na rasilimali watu kubwa na iliyoelimika,” Dk. Zhang alieleza.

Dkt Zhang aliongeza kuwa kutokana na mwenendo wa sasa wa ukuaji wa uchumi wake, Tanzania iko katika nafasi nzuri ya kupata mafanikio zaidi ikiwemo lengo la kuwa nchi ya kipato cha kati kama ilivyoelezwa katika Dira ya Taifa ya Maendeleo 2020.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents