Videos

Inasemekana kuwa TB Joshua alitabiri ushindi wa Zambia, pia juzi alitabiri kifo cha rais mmoja wa kiafrika..is he for real?? [Video]


Inasemekana kwamba anaejiita nabii kutoka nchini Nigeria, mchungaji Temitope Balogun Joshua, alitabiri ushindi wa Zambia katika mechi ya fainali ya African Cup of Nations masaa kabla ya mechi kufanyika. Alitamka maneno hayo kwa waumini wake ‘Najua kuna mechi mnayotaka kuangalia, na pia mnataka nitoe maoni yangu. Nchi ambayo haitegemewi kushinda ndio itakuwa na baraka hiyo, Mungu anataka kuwapa furaha kutokana na historia yao na matatizo waliyopitia. Leo ni siku ya kusahau mabaya, kufurahi na kucheza!’

Katika historia ya AFCON mara ya mwisho kwa team ya Zambia kufika fainali ilikuwa mwaka 1994, mwaka mmoja tu baada ya wachezaji 18 ya timu hiyo kufariki katika ajali ya ndege nchini Gabon.

Aliendelea kusema ‘Mungu amenionesha mechi nzima, na nimeona kwamba katika dakika ya 70 kutakua na kosa, mchezaji badala ya kufunga goli la wazi atapiga mpira nje’. Kwa kushangaza kweli kilitokea, mfungaji mahiri na bora Didier Drogba alikosa penalty na kupaisha mpira katika dakika ya 70!

Tukiachana na mpira inasemekana kuwa TB Joshua katika ibada yake ya Jumapili Februari 5 alitabiri kifo cha Rais mmoja wa kiafrika ndani ya miezi miwili. Wanaoamini utabiri wa TB Joshua wameanza kuhisi kwamba alikuwa anamuongelea Rasi Mugabe wa Zimbabwe, amabye anaongoza kwa uzee akiwa na umri wa miaka 88, akifatiwa na Mwai Kibaki (81), Paul Biya wa Cameroon (79) na Michael Sata wa Zambia (75).


Inasemekana kuwa TB Joshua anajulikana kwa utabiri wake wa matokeo mbali mbali kama kifo cha Michael Jackson, kujiuzulu kwa Rasi wa Pakistan Pervez Musharraf na pia ushindi wa Rais wa Ghana John Atta Mills.

Tumetafuta video za ibada ya TB Joshua lakini nyingi hazipo tena katika tovuti ya YouTube, tumepata video moja ambayo ilipandioshwa tarehe 14 Februari kwa hiyo kuthibitisha utabiri wake ni ngumu kwa sasa…wadau mnaonaje, is he for real?

[youtube]http://www.youtube.com/watch?v=vC7giIJT0pw[/youtube]

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents