Habari

India yapiga marufuku uuzaji wa pombe barabarani kuzuia ajali

Baa nyingi za nchini India zitajikuta kwenye ukata mkubwa. Tangu April 1, uuzaji wa pombe barabarani umepigwa marufuku.

Hatua hiyo imechukuliwa kuzuia idadi ya vifo vinavyosababishwa na watu kuendesha wakiwa wamelewa. Hilo ni pigo kwa baa, hoteli nyingi na vijiwe vya kuuzia ulabu katika sehemu nyingi nchini humo.

Kila baa, kuanzia zile za kifahari hadi za hali duni zilizo ndani ya mita 500 kutoka kwenye barabara kuu zote sasa hazina pombe.

Mapato zaidi ya dola bilioni 10 yatapotea kutokana na uamuzi huo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents