Habari

India yapoteza mawasiliano na chombo kilichotumwa mwezini

Shirika la anga la India limepoteza mawasiliano na chombo chake cha angani walichokirusha kwenda mwezini muda mfupi kabla ya kutua karibu na ncha ya kusini ya mwezi, likiwa pigo kubwa kwa matarajio yake ya kutua mwezini.

Indien: Chandrayaan-2 (picture-alliance/Z. Naijie)

India ilikuwa na matumaini ya kuwa taifa la nne, baada ya Marekani, Urusi na China kufanikiwa kutua mwezini. Kwa mujibu wa asasi ya utafiti wa masuala ya anga ya India ISRO, ni kwamba taifa hilo pia lilikuwa na lengo la kuwa taifa la kwanza kutua upande wa ncha ya kusini. Akizungumza katika kituo cha kukiongoza chombo hicho, mwenyekiti wa ISRO Kailasavadivoo Sivan alisema mawasiliano katika eneo la utuaji yalipotea.

Waziri Mkuu Modi azungumzia mpango wa mwezini

Hata hivyo Waziri Mkuu wa India ambae alisafiri kwenda katika kituo cha anga cha Bangalore kushuhudia hatua ya kutoa kwa chombo hicho aliwapa matumaini wanasayansi kwa kusema hatua waliofikia si ndogo. Mafanikio na kushindwa ni mambo ambayo lazima mwanadamu akumbane nayo. Akizungumza baada ya tangazo la kupotea kwa mawasiliano alitoa kauli ya matumani kwa kusema “Kama mawasiliano yataanza tena..tuna matumaini makubwa..Safari yetu itaendelea.”

Malengo ya kurushwa kwa chombo

Kwa mujibu wa shirika la habari la DW, Mradi huo ambao umegharimu Euro milioni 126 na ulilenga kulizunguka eneo la kusini la mwezi. Zaidi ya hayo, chombo hicho cha india kilikuwa na shabaha pia ya kuchunguza uwezekano wa kuwepo maji mwezini. Chombo hicho cha anga za juu cha India kilianza safari yake tangu Julai 22 iliyopita -takriban miaka 50 baada ya chombo kama hicho cha Marekani, Apollo 11, kumteremsha kwa mara ya kwanza binaadamu mwezini.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents