Burudani ya Michezo Live

India yarejesha safari zake za ndege za ndani

India imerejesha safari za ndege za ndani hii leo, licha ya kuongezeka kwa visa vya maambukizi ya virusi vya corona, huku abiria wakiingiwa na mashaka kuhusu sheria za kukaa karantini mnamo wakati safari kadhaa za ndege pia zimefutwa.

India ilisitisha safari zote za ndani ya nchi na kimataifa mnamo mwisho wa mwezi Machi kama hatua ya kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona.

 

Lakini wiki iliyopita, serikali ya taifa hilo la tatu kiuchumi katika bara la Asia, ilitangaza kuwa itaruhusu jumla ya safari 1,050 za ndege kila siku kuanza tena kuanzia leo, kama hatua ya kuanza kurejesha uchumi ambao umeathiriwa.

Serikali kadhaa za majimbo zimetangaza kuwa abiria watalazimika kukaa karantini kwa wiki mbili punde wakiwasili wanakoelekea.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW