Burudani

India yaweka rekodi kwenye mashindano ya Miss World, Waziri Mkuu atoa pongezi (+Picha)

Miss India mwaka 2017, Manushi Chhillar ametwaa taji la Miss World 2017 usiku wa kuamkia leo akiwapiku washindani wengine kutoka nchi 118 walioshiriki kwenye mashindano hayo.

Miss World 2017 kutoka India, Manushi Chhillar.

Ushindi huo wa Manushi unakuwa ushindi wa taji la sita kwa India tangu mashindano hayo yaanzishwe mwaka 1951 na kuweka rekodi kwa kuifikia Venezuela.

India sasa inaungana na Venezuela kwa utoaji wa washindi wengi zaidi 6) huku ikifuatiwa na Uingereza iliyochukua mara 5.

Ushindi wa Manushi umekuja baada ya kupita miaka 17 tangu Miss India mwaka 2000, Priyanka Chopra kutwaa taji hilo.

Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi‏ kupitia ukurasa wake wa Twitter amempongeza mlimbwende huyo kwa kuandika “Congratulations @ManushiChhillar! India is proud of your accomplishment.”

Washindi wengine wa pili na watatu kwenye mashindano hayo ni  Andrea Meza kutoka Mexico na Stephanie Hill kutoka Uingereza.

 Manushi (20) ni mwanafunzi wa medical katika chuo cha Haryana na mashindano ya Miss World mwaka huu yamefanyika katika ukumbi wa Sanya Arena mjini Sanya nchini China.Tazama picha za mshindi huyo hapa chini

Mshindi wa Kwanza katikati, wa pili na watatu kwenye picha moja.

Mshindi wa taji la Miss World 2017, Manushi Chhillar kabla ya mashindano
Washiriki wakisakata rumba kabla ya mashindano kuanza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents