Tupo Nawe

INDIAFRICA: A Shared Future for Two Billion People

Mpango maalumu wa nchi ya India wa kukuza mbinu za ushirikiana wa
kinaendeleo baina ya India na Afrika

Kwa mujibu wa Balozi Pinak Chakravarty, Katibu Maalumu wa idara ya
Umma ya Wizara ya Mambo ya Nje na Diplomasia “India na Afrika
tunaingia katika ukurasa mpya baada wa kihistoria kupitia ukoloni na
unyonyaji wa kiuchumi hadi kufikia uhuru. Na sasa uhusiano wetu
unazidi kukua kwa kasi. Uhusiano wetu huu mpya umeegemea zaidi katika
uhusiano wa kiuchumi katika dunia hii ya utandawazi.

theIdeaWorks, ni mpango maaalumu wa kibiashara ambao makao makuu yake
yako mjini Delhi, na unasimamiwa na idara maalum ya Umma, chini ya
Wizara ya Mambo ya Nje ya serikali ya India. INDIAFRICA: A Shared
Future ni mpango wa miaka mitatu na ulizinduliwa mnamo mwaka 2011.

Mpango wa P2P inakaribisha mbadilishano wa mawazo kati ya vijana
kutoka Africa na India, kupitia mfululizo wa mashindano mbalimbali ya
wajasiriamali vijana. Pia ina lengo la kujenga jukwaa la vijana
wajasiriamali kutoka India na Afrika lenye nguvu, uvumbuzi na ushindani.

“Kuongezeka kwa uwezo wa kiutamaduni, ni muhimu kwa ajili ya
mafanikio, Na kuwajenga vijana kuwa raia wazuri wa kimataifa na kukuza
ndoto na matarajio yao katika nchi yoyote duniani. Kwa mtazamo huu,
watu hasa vijana wana jukumu kubwa na muhimu la kujenga dunia na
kushikamana ili kuweza kuleta maisha bora kwa watu wote baadae, ikiwa
watu wote bilioni mbili wakijenga ndoto na historia yao kwa pamoja.”
Alisema Seema Kundra, Mkurugenzi wa theIdeaWorks.

INDIAFRICA:A Shared Future ni mpango wa kimawasiliano unaojumuisha
mashindano mbalimbali kama, uandishi wa insha, upigaji picha na
ubunifu. Hii itasaidia kujenga jukwaa la vijana kutoka Afrika na India
wenye vipaji na uwezo wa kushirikiana katika changamoto na mafanikio
yao; Na baadae kushirikiana kiubunifu, biashara na utamaduni.

Jumuia ya vijana wenye malengo na mipango ya kubainisha wajasiriamali
vijana kutoka India na Afrika, na unawapa fursa ya ukuaji na
ushirikiano. Lengo lake ni kubadilishana mawazo na kuongeza uelewa
mzuri wa changamoto na fursa za kibiashara katika pande zote mbili.

Nikimnukuu Navdeep Suri, Katibu Mkuu wa Idara ya Diplomasia na Umma,
Wizara ya Mambo ya Nje ya India alisema, “70% ya idadi ya idadi ya
watu katika bara la Afrika kwa sasa wako chini ya umri wa miaka 25,
ambapo ni takwimu zinazoshabiihana na India. Hivyo basi ni muhimu sana
kukuza ushirikiano kati ya vijana kutoka Afrika na India ili kusafisha
njia kwa ajili ya malengo ya pamoja hapo baadae. Lengo la mpango huu
ni kufanya kazi kwa pamoja ili kuibua nishati hiyo kubwa ya vijana na
kuhamasisha mawazo yao ya kipekee na yenye nguvu na ubunifu, na
kuwawezesha kuwa wawezeshaji na vichocheo vya mchakato huo.”

Katika kila kila kundi la ushindani, zawadi ya fedha taslimu ya Dola
1000 za Kimarekani kwa washindi watatu kutoka kila kanda ambazo ni
Afrika Mashariki,Afrika Magharibi,Afrika ya Kati,Kusini na India.

Kila mshindi wa shindano la vijana wenye maono, watapewa ziara ya siku
tano kati ya India au Afrika (kulingana na nchi aliyopo) ambayo
itaambatana na semina na mikutano ya kibiashara; Pamoja na muingiliano
ya kimawasiliano ya kibiashara. Washiriki wachache wa mwisho
watakaotajwa wataweza kushiriki katika shindano la dola 10,000 za
Kimarekani na kuendeleza ushirikiano kati ya India na Afrika.

INDIAFRICA itasaidia kuvunja mipaka na kukuza na kuhamasisha
ushirikiano mpya, na utambuzi wa kimataifa na kutatua matatizo ya
kirasilimali kati ya wanafunzi wa vyuo vikuu, shule za sekondari,sekta
ya viwanda, wajasiriamali na viongozi kutoka India na Afrika ili
kuweza kuukaribisha mpango huu wa INDIAFRKA.

Hivyo kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ambao kwa
sasa wanasherehekea miaka 50 ya kuanzishwa kwake pamoja na AIESEC
Tanzania,INDIAFRICA imeandaa kongamano linalojumuisha vyuo vyote
litakalofanyika mnamo tarehe 12 Mei 2012 katika ukumbi wa Nkuruma
ndani ya chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kongamano hili ni bure kabisa
kwa wanfunzi wote wa elimu ya juu, wataalamu na vijana. Washiriki wote
watapata nafasi ya kubadilishana mawazo na wajasiriamali vijana kutoka
India na Tanzania.

“Mpango huu ni jukwaa kamili la kwa ajili ya wajasiriamali vijana, kwa
ajili ya kuandaa matarajio yao ya baadae ya kazi zao. Maendeleo yetu
ya kesho, yamo mikononi mwa kijana wa leo, nami nimepata heshima ya
kuwa sehemu ya mradi huu ambao una lengo la kuleta India na Afrika kwa
pamoja hasa Tanzania ; Kuimarisha mahusiano ya nchi hizi mbili kwa
karne mbili” Alisema Mustafa Hassanali mbunifu nguli wa mavazi
Tanzania na muandaaji wa Swahili Fashion Week.

Swahili Fashion Week kwa pamoja na INDIAFRICA wanaandaa mashindano
maalumu kwa ajili ya kuleta muingiliano kwa vijana wadogo
wanaochipukia katika nyanja ya ubunifu wa mitindo nchini Tanzania,
ambapo washindi wataweza kuonyesha ubunifu wao katika maonyesho
makubwa ya mavazi Afrika mashariki na kati ya Swahili Fashion Week
yanayofanyika mwezi November kila mwaka.

“Tunatoa wito mkubwa kwa kila mtu kushiriki katika mdahalo huu wa aina
yake hapo tarehe 12 Mei 2012,ambapo hautapata nafasi ya kukutana na
vijana wajasiriamali wenye maono ya mafanikio na maendeleo tu, bali
pia hafla fupi ya muziki itakayofanywa na wasanii wanaotikisa nchini
Tanzania,” Alihitimisha Seema Kundra

Kuhusu INDIAFRICA: A Shared Future

Mpango wa INDIAFRICA umezaliwa nje ya utambuzi wa hisia za pamoja ili
kuweza kuunganisha historia na tamaduni kati ya India na Bara la
Afrika, na uhusiano wa Wahindi zaidi ya milioni mbili waishio nje ya
India.

Pia INDIAFRICA imedhamiria kutoa jukwaa kwa wanafunzi, wafanyabiashara
vijana na watu mbalimbali wenye maono ya mbali kupitia midahalo ya
pamoja.Pia kushirikiana kwa pamoja katika Nyanja ya kibiashara na
ubunifu, mpango wa INDIAFRICA ni mpango wa muda mrefu unaoendelea
ukizingatia historia na uhusiano kati ya India na Afrika

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW