Infantino amkabidhi jezi Trump, wakati rais wa taifa hilo kubwa duniani akionyesha kadi nyekundu
Rais wa Shirikisho la soka duniani (FIFA), Gianni Infantino amekutana na kufanya mazungumzo na Donald Trump kuhusiana na maandalizi ya michuano ya kombe la dunia mwaka 2026 ambayo taifa la Marekani likiwa mwenyeji kwa kushirikiana na Canada pamoja na Mexico.
Infantino alimkabidhi rais wa taifa hilo la Marekani, Trump jezi yenye jina zenye jina lake na kumkabidhi kadi mbili nyekundu na njano.
Trump ameonekana kufurahishwa mno na kikao hicho alichofanya na rais wa FIFA huku Infantino akimtania kwa kumuambie atafute rangi ya kadi itakayotumika zaidi kwenye michuano hiyo.
Rais wa FIFA anaamini kuwa michuano hiyo itakuwa ya kihistoria huku Trump akisema kuwa mwaka 2026 ambao michuano hiyo itafanyika hatukuwa rais kwakuwa kipindi chake kitakuwa kimeshamalizika.
Trump amemuita Infantino ambaye amechukua madaraka baada ya skendo za rushwa za rais Seth Blatter kuwa ni mtu mwenye heshima kubwa sana huku akizungumzia mchezo huo utakavyoitwa.
”Soka ni mchezo, nadhani mnauita mpira lakini kuanzia hapa huwenda baadhi ya mambo yakabadilika majina ila sina uhakika,” amesema Trump.
”Lakini tusubiri tuone, itafanya kazi vizuri. Ila nahitaji kukushukuru, Gianni Infantino kwa uwepo wako hapa wewe ni rais wa FIFA na mtu mwenye heshima kubwa mno.”
Nice
IPhone 5s GB32 bei 360,000/=