Michezo

Iniesta atangaza rasmi kuondoka Barcelona, machozi yamwagika hadharani

Kiungo mkongwe wa Barcelona na timu ya taifa ya Hispania, Andres Iniesta ametangaza ataondoka kwenye klabu hiyo mara baada ya msimu huu kumalizika.

Iniesta (33) amedumu ndani ya Barcelona tangu mwaka 1996 alipojiunga na timu ya vijana, tayari mpaka sasa ameshachukua vikombe 31 akiwa na timu hiyo.

Mchezaji huyo alianza kuichezea timu ya wakubwa ya Barca 2002 na amecheza mechi 669 wakati kipindi hicho akiwa na umri wa miaka 18.

Iniesta ametangaza maamuzi hayo huku akitokwa na machozi leo katika mkutano wake ambao ulihudhuriwa na mbele ya mkewe na watoto wake, baadhi ya wachezaji wenzake wa Barca na rais wa timu hiyo Josep Maria Bartomeu.

Kiungo huyo anatarajiwa kujiunga na Chongqing Dangdai inayoshiriki ligi kuu ya China. Hata hivyo klabu ya Manchester City imeonekana kumuhitaji mchezaji huyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents