Aisee DSTV!

IRAN: Vikwazo vipya vya Marekani vyaelekezwa kwa kiongozi mkuu wa dini 

Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa anaiwekea vikwazo vikali Iran ikiwemo afisi ya kioingozi mkuu wa dini Ali Khamenei.

Rais Donald Trump

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Bwana Trump amesema kuwa vikwazo hivyo vya ziada ni kujibu hatua ya Iran kuiangusha ndege isio na rubani ya Marekani na mambo ‘mengine mengi’.

Ayatollah Khamenei , ambaye ndio kiongozi mkuu nchini Iran alilengwa kwa kuwa ndiye anayehusika na hali ya uhasama katika utawala wa taifa hilo.

Waziri wa maswala ya kigeni nchini humo Mohamed Javd Zarif alisema kuwa Marekani haipendelei diplomasia.

Katika ujumbe wa Twitter kufuatia tangazo la rais Trump, bwana Zarif pia aliushutumu utawala wa Trump kwa kuwa na kiu ya vita

Hali ya wasiwasi kati ya mataifa hayo mawili imekuwa ikipanda katika wiki za hivi karibuni.

Hatahivyo waziri wa fedha nchini Marekani Steve Mnuchin alisema kuwa maagizo ya rais Trump ambayo yatazuia mabilioni ya madola ya mali ya Iran yalikuwa yanaandaliwa hata kabla ya Iran kuiangusha ndege ya Marekani isiokuwa na rubani katika Ghuba wiki iliopita.

Je ni nani anayeathiriwa?

Wizara ya fedha nchini Marekani imesema kuwa makomanda wanane wa Iran ambao husimamia kitengo kinachoshauri vitendo vya jeshi kuu la {Islamic Revolution Guard Corps} IRGC walikuwa wanalengwa katika vikwazo hivyo vipya.

Iliongezea kuwa agizo la rais Trump pia litaunyima uongozi wa Iran kupata raslimali za kifedha mbali na kuwalenga watu walioajiriwa na kiongozi huyo wa dini katika afisi kadhaa ama nyadhfa tofauti mbali na taasisi za kigeni za kifedha ambazo huwasaidia kufanya biashara.

Marekani imedai kwamba Ayatollah Khamenei ana utajiri mkubwa ambao unafadhili jeshi la IRGC.

Mwaka 2018 waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Mike Pompeo alisema kwamba kiongozi huyo ana utajiri wenye thamani ya $95b ambao hutumika kulifadhili jeshi hilo.

Vikwazo pia vitamlenga waziri wa maswala ya kigeni bwana Javad Zarif baadaye wiki hiki , kulingana na bwana Mnuchin.

Kwa nini Marekani inaweka vikwazo?

Mnamo mwezi Mei 2018, Ikulu ya Whitehouse ilirejesha vikwazo vyote ambavyo vilikuwa vimeondolewa dhidi ya Iran chini ya mkataba wa kinyuklia wa Iran ambao uliafikiwa na viongozi wa mataifa yenye uwezo mkubwa duniani ili kuizuia Iran kutengeza silaha zake za Kinyuklia.

Uhusiano kati ya mataifa hayo mawili uliharibika mnamo mwezi Mei -mwaka mmoja baada ya bwana Trump kujiondoa katika mkataba huo wa Kinyuklia , Marekani ilianzisha shinikizo dhidi ya Iran kwa kuziondolea ruzuku nchi ambazo zinanunua mafuta kutoka Iran.Vikosi vya Marekani Ghuba

Hatua hiyo ilifuatiwa na mashambulizi dhidi ya meli za mafuta katika Ghuba , ambayo Ikulu ya Whitehouse inasema kuwa Iran ndio ya kulaumiwa.

Tehran hatahivyo imekana madai hayo. Baadaye Maafisa wa Iran walisema kuwa taifa hilo litakiuka dhidi ya kiwango cha uzalishaji wa madini ya uranium yanayotumika kutengenezea silaha za kinyuklia.

Siku chache baadaye , ndege ya Marekani isiokuwa na rubani ilishambuliwa na majeshi ya Iran na kuangushwa katika kile ambacho Marekani inasema ni maji ya kimataifa , lakini Iran inasema kuwa ndege hiyo ilikuwa katika himaya yake.

Je vikwazo vya awali vimeiathiri vipi Iran?

Vikwazo hususan vile vilivyowekwa dhidi ya nishati , meli na sekta za kifedha -vilisababisha uwekezaji wa kigeni kupotea na kuathiri uuuzaji wa mafuta.

Vinazuia kampuni za Marekani kufanya biashara na Iran, mbali na kampuni za kigeni au mataifa yanayofanya biashara na Iran.Ayatollah Khamene

Hatua hiyo imesababisha uhaba wa bidhaa za kutoka nje ambazo hutengezwa na mali asli kutoka ugenini hususan nguo za watoto.

Kunaguka kwa thamani ya sarafu ya taifa hilo pia kunaathiri gharama ya chakula kutoka nchini humo kama vile nyama na mayai ambazo zimepanda bei.

Iran imejibu shinikizo hizo za Marekani kwa kusema kuwa inapanga kukiuka baadhi ya makubaliano ya mkataba wa kinyuklia.

Pia Iran imelaumu mataifa ya Ulaya kwa kushinda kuheshimu ahadi zake za kulinda uchumi wa taifa hilo dhidi ya vikwazo vya Marekani.

Je ndege isiokuwa na rubani ilifanywa nini?

Jeshi la Iran la IRGC lilisema kuwa kuangushwa kwa ndege hiyo isiokuwa na rubani ilikuwa ujumbe wazi kwa Marekani kwamba mipaka ya Iran ni hatari.

Lakini jeshi la Marekani linasisitiza kuwa ndege hiyo isiokuwa na rubani ilikuwa katika anga ya kimataifa katika mkondo wa bahari ya Hormuz wakati huo.

Amir Ali Hajizadeh , afisa mkuu katika jeshi la IRGC alisema kuwa ndege nyengine ya kijeshi iliokuwa ikibeba abiria 35 ilikuwa ikiruka karibu na ndege hiyo.

”Pia tungeiangusha hiyo pia, lakini hatukufanya hivyo”, alisema.Eneo ambalo ndege isiokuwa ya rubani inadaiwa kuangushwa

Eneo ambalo ndege isiokuwa ya rubani inadaiwa kuangushwa

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW