Habari

Iran yakataa msaada wa Marekani, yadai virusi vya Corona vilianzishwa na taifa hilo

Kiongozi Mkuu wa kidini nchini Iran, Ayatollah Ali Khamenei amesema Iran haitopokea msaada wowote kutoka Marekani, katika kubadili hali ilivyo kutokana na wimbi la maambukizi ya virusi vya corona nchini mwake.

Image result for Iran leader refuses US help, citing virus conspiracy theory

Katika taarifa yake hiyo Khamenei alirejea kuizungumzia dhana ya kwamba virusi hivyo ni silaha iliyoundwa na Marekani dhidi ya maadui zake.

Katika hotuba yake iliyorushwa moja kwa moja kupitia televisheni kiongozi huyo amesikika akisema wana maadui wengi lakini, mkubwa kuliko wote ni Marekani na sasa anataka kuwasaidia. Ni vyema taifa hilo likajikita katika kuwasaidia wananchi wake.

Iran limekuwa eneo tete la usambaaji wa virusi vya corona, ambavyo vilianzia China mwishoni mwa mwaka uliopita. Hata hivyo usambaaji wa visa hivyo ulianza kuingia Marekani wiki iliyopita.

Marekani inakabiliwa na mamia ya vifo vyenye kuhusishwa na virusi hivyo, wakati Iran vifo vyake vinapindukia watu 1000.

Katika hatua hiyo ya kukataa msaada, Khamenei aligusia nadharia ya kwamba virusi hivyo viliundwa na Marekani kwa lengo la kuyadhoofisha mataifa adui kama China na Iran.

Tangu Januari Khamenei amekiwa akisema virusi hivyo vinaweza kuwa silaha ya kibailojia iliyoundwa na Marekani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents