Burudani ya Michezo Live

Iran yatoa vitisho vya kivita ‘Tupo tayari kupigana na Saudi Arabia na vibaraka wao Marekani’

Kufuatia shutuma zinazotolewa na Marekani kuwa Iran ndio imetekeleza tukio la kushambulia vituo viwili vikubwa vya mafuta nchini Saudi Arabia vya Saudi Aramco na Khurais, Iran imesema ipo tayari kwa lolote lile hata ikibidi kwa vita endapo mataifa hayo mawili yataendelea kuwachokoza.

Jana Septemba 14, 2019 Shambulio la ndege zisizokuwa na rubani zimerusha mabomu katika hifadhi vituo hivyo vikubwa vya mafuta ambavyo vinazomilikiwa na kampuni ya serikali ya taifa la Saudi Arabia.

Kanda za video zilizovuja mitandaoni zinaonesha moto mkubwa katika eneo la Abqaiq ikiwa ndio hifadhi kubwa ya mafuta ya Saudia huku shambulio la pili likichoma moto hifadhi ya mafuta ya Khurais.

Tayari, Msemaji wa kundi la waasi la Houthi la nchini Yemen, Limesema kuwa ndio limetekeleza shambulio hilo kwa kurusha ndege 10 zisizo na rubani.

Msemaji waasi hao, Yahya Sare akiongea na kituo cha runinga cha al-Masirah, Ambacho kinamilikiwa na waasi hao amesema kuwa mashambulizi zaidi yanafuata katika siku za usoni.

Sare amesema shambulio hilo la jana ndio kubwa zaidi kuwahi kutekelezwa na wapiganaji hao ndani ya Saudi Arabia na kwamba lilitekelezwa kupitia usaidizi wa baadhi ya raia wa nchi hiyo.

Kundi hilo ambalo linapewa nguvu na Iran na baadhi ya Raia wa Yemen na Saudi Arabia, Limepelekea Marekani kutangaza kuwa Iran ndio iliyotekeleza shambulizi hilo.

Maafisa nchini Iran wamesema hao wapo tayari kwa lolote lile hata ikiwezekana vita dhidi ya Saudi Arabia na vibaraka wao Marekani, Endapo watawachokoza.

Hata hivyo, Maafisa usalama nchini Saudi Arabia mpaka sasa hawajatoa tamko lolote lile kuhusu shambulizi hilo, Ukiachilia mbali Marekani inayoonekana kushupalia tukio hilo.

Saudi Arabia ni moja ya mataifa ya Mashariki ya Kati yenye urafiki mkubwa wa kidiplomasia na kibiashara na taifa la Marekani.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW