Iran yatoa wanrati kukamatwa kwa Trump

Iran yatoa wanrati kukamatwa kwa Trump

Iran imetoa waranti wa kukamatwa na imeliomba msaada shirika la polisi ya kimataifa Iterpol kumkamata Rais Donald Trump na wengine kadhaa inaoamini walifanya shambulio la ndege isiyo na rubani lililomuuwa jenerali wa juu wa Iran mjini Baghdad.

It is unlikely Interpol would grant Iran's request as its guideline for notices forbids it from 'undertaking any intervention or activities of a political' nature. [Reuters]

Mwendesha mashtaka wa Tehran Ali Alqasimehr amesema Trump na watu wengine zaidi ya 30 ambao Iran inawatuhumu kwa kushiriki katika shambulio la Januari 3 lililomuuwa Jenerali Qassem Soleiman mjini Baghdad, wanakabiliwa na mashtaka ya mauaji ya ugaidi.

Alqasimehr hawakuwataja wengine wanaotafutwa mbali ya Trump, lakini amesisitiza kuwa Iran itaendelea kufuatilia mashtaka dhidi yake hata baada ya kukamilika kwa muhula wake wa urais.

Shirika la Interpol lenye makao yake nchini Ufaransa, halikujibu maombi ya kuzungumzia suala hilo. Ingawa Trump hayuko katika hatari yoyote ya kukamatwa, mashtaka hayo yanaonyesha mzozo unaozidi kati ya Iran na Marekani tangu Trump alipoitoa Marekani kwenye mkataba wa nyuklia kati ya Iran na mataifa makubwa.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW