Habari

Iraq yafanya maandamano kuishinikiza Marekani iondoke

Maandamano makubwa yamefanyika karibu na Ubalozi wa Marekani Mjini Baghdad, kutaka Vikosi vya nchi hiyo kuondolewa Iraq.
Wananchi Iraq wakiwa katika maandamano


Hii ni baada ya Kiongozi wa dhehebu la Shia, Moqtada al-Sadr kuwataka Raia wa nchi hiyo kushiriki maandamano hayo kwa wingi

Bunge la Iraq lilipiga kura ya kuwaondoa wanajeshi wa Marekani baada ya kifo cha Jenerali Qasem Soleimani kilichotokea Januari 3 mwaka huu, lakini uongozi wa Rais Trump ulisema hautaondoa majeshi yao nchini humo

Uamuzi wa Marekani kumuua Soleimani ulikosolewa vikali na Iraq, na Raia wengi wa Nchi hiyo wamekuwa na hofu kuwa Taifa lao linaweza kuwa katikati ya vita vya Marekani na Iran

Na Jacquiline Ngoya

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents