Irene Afunga Ndoa

Irene Afunga Ndoa
Msanii maarufu wa kike wa filamu na mlimbwende aliyeshinda nafasi ya 5
katika miss Tanzania 2005/2006 Irene Uwoya amefanikiwa kufunga ndoa na
mpenzi wake wa kinyarwanda bwana Hamad Ndikumana anaejulikana kama Kataut

Ndoa hiyo ambayo ilifungwa jumamosi ya tarehe 11 ya mwezi wa saba katika kanisa la Mtakatifu Joseph imeweza kumaliza utata wa nani ni mmiliki wa mrembo huyo ambao umekuwa ukiibuka kwa muda mrefu kwenye magazeti hivyo kufungua ukurasa mpya katika maisha ya mrembo huyo.

Sherehe ya kuwapongeza maharusi iliyofanyika katika hoteli ya Giraffe mbezi ambayo ilihudhuriwa na watu wapatao 500 huku Ray, Dotnata, Dick Chen, Jebi Maimartha na mastaa wengine kibao wa muvi za kibongo.

Wanandoa hao wawili wanategemewa kuondoka jumatatu ya tarehe 13 kuelekea nchini Cyprus ambako ndio makazi ya bwana Ndikumana kikazi.

Bongo5 Inapenda kuwatakia maisha mema na marefa bwana Hamad Ndikumana katende na Irene Pankras Uwoya.

Video za harusi hiyo zitawajia baada ya muda mfupi…

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents