Habari

Irene Uwoya atoa sababu kwanini alikosa ubunge CCM

Malkia wa filamu nchini, Irene Uwoya ameweza kutoa ufafanuzi wa kutopitishwa na chama chake cha CCM kuwa mbunge wa Viti Maalum kwa wanawake.

Uwoya ameeleza hayo wakati akijibu maswali ya mashabiki wake live kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV, ambapo swali moja lilihoji sababu za yeye kutemwa kwenye ubunge ndani ya CCM na kama bado ana ndoto za kuwa mbunge.

Uwoja alisema, “Niligombea kupitia upande wa vijana na nilishinda na sisi vijana tunapigiwa kura na wajumbe, sikushindwa wala sikutemwa, kwanza kwa mkoa wa wangu wa Tabora nilipata kura za kutosha tena nilikuwa namba moja kabisa, kwenye taifa pia nilifanikiwa kuwa kwenye majina 10 ambayo yalikuwa yanategemea kura za Rais, kama Rais angepata kura nyingi basi tungechukuliwa wote.”

“Lakini kwa kura alizopata Rais ilibidi wachukuliwe 6,kwa maana hiyo asilimia hazikutosha na ndiyo maana nikabaki, kwahiyo mimi sikushindwa nilishinda lakini asilimia za kura za Rais ndiyo hazikutosha na kama unavyoona ushindani ulikuwa mkubwa sana.”

By: Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents