AFCON 2019 Tupogo!
Vodacom Data Datani!

Irene Uwoya na Dogo Janja wafunga ndoa?

Muigizaji wa Filamu nchini Tanzania, Irene Uwoya jana Jumamosi amethibitisha kuwa amefunga ndoa, huku akiwaacha watu njia panda  kwa kutoweka wazi mwanaume aliyefunga nae ndoa.

Irene Uwoya

Wikiendi hii Irene Uwoya kupitia ukurasa wake wa Instagram amekuwa bize kuposti picha zake akiwa ndani ya shela huku akimshukuru Mungu kwa kufanikisha zoezi hilo.

Licha ya Irene Uwoya kutomtaja mwanaume, marafiki zake wa karibu wamempongeza na kumtaja mwanaume huyo kuwa ni Dogo Janja.

Mtu wa kwanza kutoa pongezi kwa Irene Uwoya ni Mtangazaji wa Clouds TV, Zamaradi Mketema ambapo amemtaja Dogo Janja kwenye pongezi hizo kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuandika “Hongera Sana kwa NDOA mpenzi wangu, mwanzo nilihisi ni movie lakini sasa nimeamini.. MUNGU awatangulie katika hili mlilolifanya @ireneuwoya8 @dogojanjatz kila la kheri INSHA’ALLAH!!

Hata hivyo licha ya kuzagaa kwa taarifa hizo mitandaoni kuwa wawili hao wamefunga ndoa bado Dogo Janja hajatoa taarifa yoyote kuhusu tetesi hizo.

Watu wa karibu na Dogo Janja wamekanusha taarifa hizo lakini Madee kwenye mahojiano yake mafupi na Bongo5 amethibitisha kuwa mwanaye Dogo Janja amefunga ndoa na harusi yake imefanyika Ijumaa ya wikiendi hii.

Posti ya Madee aliyoiweka mapema leo asubuhi kwenye mtandao wa Instagram

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW