Burudani

Irene Uwoya na Mobetto washikwa pabaya na TCRA, waomba radhi kama walivyoagizwa

Kamati ya maudhui ya mamlaka ya mawasiliano (TCRA) imewataka wasanii Hamisa Mobeto na Irene Uwoya kuomba radhi kwa kosa la kuweka picha za utupu mtandaoni.

Uamuzi huo uliochukuliwa baada ya wasanii hao kukiri kosa, umetangazwa leo Alhamisi Julai 19, 2018 mbele ya waandishi wa habari.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Vareli Msoka akiwa sambamba na wasanii hao amesema kutoka na kosa hilo wametakiwa kuomba radhi kupitia kurasa zao za kijamii na kuwa mabalozi kuhamasisha wenzao.

Kwa mujibu kamati hiyo, Hamisa alifanya kosa la kuweka mtandaoni picha za ujauzito na Irene kuweka picha zake za nusu utupu, akiwa ufukweni.

Kufuatia kosa hilo, Hamisa amepewa onyo na kutakiwa kuomba radhi kwa kuweka tangazo kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram.

Baada ya onyo hiyo, Irene Uwoya aliandika…

Wapenzi Wangu …ndugu zangu…wakubwa zangu na wadogo zangu naomba radhi kwapicha niliyopost…najua niliwakwaza mnisamehe sana sikujua ntawakwaza nisababu tu ya role model Wangu beyonce!!!nimejifunza Sasa!!!nawapenda 😘😘😘

Naye Hamissa ameandika….

NAOMBA RADHI KWA UMMA:

Husika Na Kichwa Cha Habari Hapo Juu.

Mimi Hamisa Mobetto
Ambaye ni Mfanya Biashara Wa Mitindo (Fashion Entrepreneur) Apa Nchini Tanzania Na Pia Ni Raia Wa Tanzania 🇹🇿 Naomba Kutumia Fursa Hii Kuomba Radhi Kwa Watanzania na Wengine Wote Ambao Ni Watumiaji Wa Mitandao .
Kuhusiana Na Kitendo Cha Mimi Na Washabiki Zangu (Fans) Wangu Kutuma Picha Zangu Zinazoonyesha Nusu Utupu Kwenye Page Zao Za Instagram.
.
Pia Natumia Fursa Hii Kuwashukuru Kamati Ya Maudhui Kwa Jinsi Walivyonita Kwenye Kamati Yao Na Kunipa Nafasi Ya Kujitetea Na Mwisho Kufanya Uamuzi Wenye Haki Kwangu Na Kwa Wapenzi (fans) Wangu Wote . Ninawashukuru Sana.🙏🏾
.
Mwisho Kabisa Niwahusie Vijana Wenzangu Kuepuka Kutumia Mitandao Ya Kijamii vibaya Kwani Kwa Sasa Kuna Sheria Kali Zinazokataza Picha Mbaya kutumwa Kwenye Mitandao .Naomba Pia Wapenzi (fans)Wangu Kuanzia Sasa Kutuma Picha Zangu Zenye Staha Au Kutumia Biashara Zangu Kunisapoti.
.
Nawashakuru Sana Na Mbarikiwe Sana.❤️🙏🏾

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents