Burudani

Irene Uwoya: Ndoto yangu ilikuwa kuwa rubani wa ndege

Muigizaji wa filamu, Irene Uwoya amesema uigizaji wa filamu umeharibu mipango yake ya miaka mingi ya kutaka kuwa rubani wa ndege.

uwoya

Akiongea na East Africa Radio, Uwoya alisema miaka yote aliyokuwa akisoma lengo lake kubwa lilikuwa ni kuja kuwa rubani wa ndege kwakuwa ndio kazi aliyokuwa akiipenda na alianza kusoma masomo ambayo aliamini moja kwa moja yangeweza kumfanya kufikia ndoto hizo.

Hata hivyo alisema ndoto yake hiyo ilikatika baada ya kuanza kufanya filamu na hivyo kujikuta maisha yake yakitawaliwa na filamu.

Muigizaji huyo ambaye ni mama wa mtoto mmoja, alisema pamoja na hivyo kupitia filamu amefanya mambo mengi ikiwemo kuishi maisha yake ayatakayo pasipo kumtegemea mtu yoyote. Pia amedai kuwa filamu zimwezesha kujenga nyumba ambayo anadai itakamilika muda si mrefu.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents