Burudani

Ishu ya Dayna kutusua kupitia beat ya simu

Msani wa muziki wa Bongo Flava, Dayna Nyange amesema ngoma yake ya kwanza kumtoa kimuziki ‘Mafungu’ alianza kuirekodi/kuandika kwa kusikiliza beat kupitia simu.

Hitmaker huyo wa ngoma Komela na Chovya alifanya hivyo akiwa nyumbani na ni katika kipindi ambacho alikuwa katika harakati za kuachana na muziki wa rap na kuingia katika kuimba.

“Nakumbuka wimbo niliofanya na Marlaw, verse ya pili ni verse ambayo niliandika nikiwa peke yangu usiku beat sina, beat nilikuwa naisikilizia kwenye simu fulani zile zamani zikipiga hapa mpaka nyumba ya jirani unasikia” Dayna ameiambia Bongo5.

“Kwa hiyo ule utunzi wa verse ya pili peke yangu na ndio nilikuwa mgeni sana kwenye uandishi hasa wa kuimba na melody ni kama kitu kilikuja kikanivaa na kuniambia andika hivi” amesisitiza.

Ameendelea kwa kusema baada ya kufanya hivyo alienda studio kwa Marco Chali na kumueleza hatua hiyo alisita kidogo kumpa nafasi kutokana wakati huo Marlaw hakuwepo ila nafasi fupi aliyokuja kupewa baadae ndio ikawa tiketi ya kutokea. Ngoma hiyo ilitoka mwaka 2009.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents