Habari

Israel, Umoja wa Falme za Kiarabu wafikia patamu

Israel na Umoja wa Falme za Kiarabu, UAE, zimekubaliana juu ya utaratibu wa kusafiri baina yao bila kuhitaji viza leo, wa kwanza kati ya Israel na taifa la Kiarabu, ukisainiwa wakati ujumbe wa kwanza rasmi wa maafisa wa UAE, Emarati, ukiwasili mjini Tel Aviv.

Israel, UAE agree on visa-free travel: Netanyahu - CGTN

Ziara ya ujumbe huo, iliyosifiwa kama siku nzuri ya amani na waziri mkuu Benjamin Netanyahu, imekuja baada ya Israel na UAE kuafikiana kurekebisha uhusiano wao katika makubaliano yaliyosainiwa ikulu ya Marekani mwezi uliopita.

Israel, UAE agree on visa-free travel for nationals: Netanyahu – The Dubai  Headlines

Wakati ambapo chumi zao zimeathiriwa vibaya na janga la virusi vya corona, Israel na UAE zinatazamia manufaa ya haraka kutokana na makubaliano ya kurekebisha uhusiano baina yao – ambayo yalivunja muafaka wa miaka kadhaa wa mataifa ya Kiarabu kwamba hakupaswi kuwa na uhusiano na taifa hilo la Kiyahudi hadi lifikie amani na Wapalestina.

Emarati ilikuwa nchi ya tatu ya Kiarabu kuanzisha uhusiano na Israel, na kufuatiwa muda mfupi na Bahrain. Nchi nyingine zenye uhusiano na Israel ni Misri na Jordan.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents