Burudani ya Michezo Live

ITALIA: Kocha afukuzwa kazi kwa timu yake kushinda goli 27-0

Katika historia ya mpira wa miguu duniani, Mara nyingi kocha hufukuzwa  baada ya kufanya vibaya lakini sio kwa Kocha wa timu ya soka ya vijana ya  Invictasauro ya nchini Italia ambaye amefukuzwa baada ya timu yake kuwafunga wapinzani wao goli 27-0.

Rais wa Klabu hiyo,  Paolo Brogelli, amesema ushindi huo ni wa udhalilishaji na haukuwa na lengo la watoto hao wa upinzani kujifunza hivyo uongozi wa timu umeamua kumfuta kazi kocha huyo.

“Wapinzani wetu lazima waheshimiwe, Mimi kama Rais wa timu kuna vitu sijaviona uwanjani leo. Kufunga magoli mengi ni udhalilishaji, Mbali na magoli, Nilitegemea kuona watoto wanaelimishwa zaidi uwanjani kuliko kufunga magoli tu,Hicho kitu leo sijakiona, Makocha wanatakiwa kuwafundisha wachezaji wao nidhamu, “amesema Brogelli kwenye mkutano wake na waandishi wa habari.

Klabu hiyo inayotokea Grosseto mjini Tuscany, Italian ilipata ushindi huo jana Jumamosi dhidi ya Marina Calcio  na kocha huyo alitimuliwa siku hiyo hiyo.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW