Michezo

Italia ya mtimua kocha wake, Giampiero Ventura

Italia imeamua kuachana na kocha wake, Giampiero Ventura baada ya mabingwa hao mara nne kushindwa kufuzu michuano ya kombe la dunia kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1958.

The Azzurri imepoteza mchezo wake wa mwisho dhidi ya timu ya taifa ya Sweden na kufanya kuwa mwisho wa kocha Ventura mwenye umri wa miaka 69 ndani ya kikosi hicho.

Ventura amesema rekodi yake ni bora zaidi ndani ya timu hiyo ukilinganisha na miaka 40 iliyopita.

“Nimepoteza michezo miwili tu ndani ya miaka miwili,” Ventura alikiambia kipindi cha luninga cha Italia kinachojulikana kama Le Iene siku moja kabla ya Shirikisho la soka la nchi hiyo kumuachisha kazi siku ya Jumatano.

Ventura alichukua nafasi ya Antonio Conte mwezi June mwaka 2016 na kutambulishwa kama “master of football” na rais wa Shirikisho la soka nchini Italia, Carlo Tavecchio.

“Nawaomba radhi mashabiki wa Italia kwa matokeo mabovu tuliyopata kwakuwa nafahamu kilikuwa nikitu muhimu kwao,” amesema kocha huyo wazamani wa klabu ya Napoli na Sampdoria baada ya matumaini ya kwenda kombe la dunia kupotea.

Mkataba wa kocha huyo ulikuwa ni wa miaka miwili ambapo ungefikia tamati hadi mwishoni mwa fainali za Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents